Habari

MAKAMO WA PILI ATOA AGIZO UJENZI WA MITARO

     Makamu wa Pili wa Rrais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleima Abdulla amewaagiza Wakandarasi na Wasimamizi wa Ujenzi wa Mtaro wa dharura unaojengwa katika Eneo la Kibonde Mzungu kuhakisha unakuwa na Viwango vilivyokusudiwa.

     Akikagua maendeleo ya Mtaro  na Bwawa linalotuwama maji ya mvua Fuoni Jangamizi Wilaya ya Magharibi “b”  Mhe .Hemed amesema hatua hiyo itasaidia maji kupita vizuri na kuwaondolea kero Wananchi wanaoishi katika Maeneo hayo na maeneo Jirani hasa wakati wa mvua za masika.

DKT.MWINYI AENDELEA KUPOKEA MKONO WA POLE

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameendelea kupokea salamu za pole kutoka kwa Viongozi Wastaafu, Serikali, Ndugu na Jamaa. 

     Hatua hiyo inafuatia Kifo cha Baba ake na Rais Mstaafu Marhum Hayati Ali Hassan Mwinyi.

DKT. HUSSEIN MWINYI AMEPOKEA SALAMU ZA POLE

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amepokea Salamu za Pole  kwa Viongozi Wakuu na Viongozi Wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Viongozi wa Vyama vya siasa.

Waliotoa Salam za Pole ni Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dotto Mashaka Biteko, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah na baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA UBALOZI WA OMAN KATIKA KUHIFADHI NA KUTUNZA KUMBUKUMBU

Waziri  wa Utalii na mambo ya kale Zanzibar Mhe Mudriki Ramadhan Soraga amesema wataendelea kushirikiana na Ubalozi  wa  Oman katika kuhifadhi  na kutunza kumbukumbu za Serikali na kurudishia  hadhi   ya maeneo  ya  Kihisoria ili yawe na muanekano unaovutia kwa Wageni wanaoingia Nchini na hata kwa wenyeji.

Akitembelea eneo la    Makaburi ya Wafalme yaliyojengwa  na  Sayyid Sayyid Waziri Soraga amesema  watahakikisha  wanayahifadhi  ili kuwa  sehenu muhimu ya Kihistoria.

TAASISI YA MWANAMKE INITIATIVES INA MCHANGO MKUBWA KUSAIDIA SERIKALI

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Mhe Lela Mohamed Mussa, amesema, Taaisisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF)  ina mchango katika kusaidia Serikali na kusaidia upatikanaji wa matokeo  katika Mitihani  ya Taifa Zanzibar.

Amesema katika Uongozi wao wamekuwa Mstari wa mbele kusaidia ikiwemo kutatua matatizo  yanayowakabili Wanafunzi na kuwaandalia Kambi maalum ya masomo jambo ambalo limesababisha kupatikana Matokeo mazuri katika Mitihani yao ya Taifa.

MADAKTARI WAFANYA UCHUNGUZI BAADA YA WATU KUFARIKI KISIWA PANZA

Watu Saba wamefariki Dunia na wengine 20 wanapatiwa Matibabu katika Hospitali ya Abdulla Mzee na Madaktari wanafanya Uchunguzi wa Ugonjwa usiojulikana.

Kufuatia tukio hilo Mganga Mkuu Wilaya ya Mkoani Dr. Haji Bakar Haji amesema tayari Madaktari wameanza uchunguzi kubaini chanzo na aina ya Ungonjwa atika Kisiwa hicho.

MAHAKAMA KUTUMIA MIFUMO KIDIGITAL DK.SAMIA AELEZA

    Raisi wa Jamuhuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inaendelea kuunga mkono Mahakama katika kutumia Teknolojia na mifumo ya Kidigitali. 

    Akizungumza katika Ufunguzi wa Mkutano wa Nchi 56 Wanachama wa Jumuiya ya Madola katika Ukumbi wa Golden Tulip U/ndege Dkt. Samia amesema ni muhimu kwa Sekta za kisheria kutumia teknolojia ili kuhakikisha urahisi na ufanisi katika upatikanaji wa haki kwa wote.

UOMBAJI WA VIBALI VYA SAFARI ZA NJE UTAONDOSHA USUMBUFU KATIKA UTENDAJI KAZI.

Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Muhandisi Zena Ahmed Said amesema mfumo wa uombaji wa Vibali kwa njia ya Kidigitali kwa  safari za Nje ya Nchi  utaondosha upatikanaji wa Vibali kwa wakati Nchini.

Mhandisi Zena amesema hayo huko katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha Gombani Kisiwani Pemba wakati akifungua Mafunzo ya Siku Tatu ya kujenga uelewa wa juu matumizi ya  Mfumo wa maombi ya Vibali vya Nje ya Nchi kwa Maafisa Wadhamini na Waratib wa Ofisi za Serikali Kisiwani Pemba.

MRADI WA RADIC UTASAIDIA KUIMARISHA MIPANGO YA MAENDELEO YA VYUO VIKUU

Naibu Makamu Mkuu Utawala Mipango na Fedha Chuo Kikuu cha Taifa SUZA dkt. Hashim Hamza Change amesema kuwa Mradi wa Radic utasaidia kuimarisha mipango ya maendeleo ya Vyuo Vikuu Saba viliopo katika Mradi huo.

Dkt. Hashim amesema RADIC utasaidia kupata Elimu Watu wote wakiwemo wenye Ulemavu kwa kutumia Teknolojia ya kisasa, Mitaala na Vifaa vya kufundishia.

Meneja Mradi wa RADIC Kari-pekky Murtorav akizungumzia Mradi huo amesema ni kwa Nchi za Afrika Mashariki hasa kwa Watu wenye Ulemavu na hata kutoa huduma kwa wote.

WANANCHI KUPATA MATIBABU BURE KAMPENI YA AFYA BORA MAISHA BORA.

Jumla ya Shilingi Bilioni 1 Nukta 5 zinatarajiwa kutumika katika Kampeni maalum ya afya bora Maisha bora kwa kuwapima na kupata Matibabu bure Wananchi wenye Magonjwa mbalimbali kwa Zanzibar.

Akizungumza katika Viwanja vya Hospitali ya Kivunge wakati wa ufunguzi wa Kambi ya Siku 5, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Rashid Hadid Rashid amesema Serikali inatumia gharama kubwa kuwapeleka Wagonjwa Nje kupata Tiba hivyo Kampeni na Kambi hizo zitapunguza hali hiyo kwa kiasi kikubwa.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.