SERIKALI KUSHIRIKIANA NA UBALOZI WA OMAN KATIKA KUHIFADHI NA KUTUNZA KUMBUKUMBU

WAZIRI WA UTALII NA MAMBO YA KALE ZANZIBAR

Waziri  wa Utalii na mambo ya kale Zanzibar Mhe Mudriki Ramadhan Soraga amesema wataendelea kushirikiana na Ubalozi  wa  Oman katika kuhifadhi  na kutunza kumbukumbu za Serikali na kurudishia  hadhi   ya maeneo  ya  Kihisoria ili yawe na muanekano unaovutia kwa Wageni wanaoingia Nchini na hata kwa wenyeji.

Akitembelea eneo la    Makaburi ya Wafalme yaliyojengwa  na  Sayyid Sayyid Waziri Soraga amesema  watahakikisha  wanayahifadhi  ili kuwa  sehenu muhimu ya Kihistoria.

Balozi mdogo wa Omani kutoka Zanzibar Said Salimu Alsinawi amesema wataendelea kushirikiana katika  mambo mbalimbali ya Kihisoria  ili kuinua  Secta ya Utalii Nchini. 

Akisoma Risala  inayohusiana na ushirikiano wao  Mwenyekiti wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu kutoka Omani Hemedi  Bin Muhammed Al dhayan amesema lengo la ziara hiyo ni kuhakikisha Nchi mbili hizo zinakuwa karibu katika masuala mnali mbali hasa ya utamaduni na Historia.

Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na mambo ya Kale  Fatma Mabrouk Khamisi  amesema  hatua hiyo itawasaidia kusoma kwa Histori hasa za Wafalme waliopita.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.