Waziri wa Utalii na mambo ya kale Zanzibar Mhe Mudriki Ramadhan Soraga amesema wataendelea kushirikiana na Ubalozi wa Oman katika kuhifadhi na kutunza kumbukumbu za Serikali na kurudishia hadhi ya maeneo ya Kihisoria ili yawe na muanekano unaovutia kwa Wageni wanaoingia Nchini na hata kwa wenyeji.
Akitembelea eneo la Makaburi ya Wafalme yaliyojengwa na Sayyid Sayyid Waziri Soraga amesema watahakikisha wanayahifadhi ili kuwa sehenu muhimu ya Kihistoria.
Balozi mdogo wa Omani kutoka Zanzibar Said Salimu Alsinawi amesema wataendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali ya Kihisoria ili kuinua Secta ya Utalii Nchini.
Akisoma Risala inayohusiana na ushirikiano wao Mwenyekiti wa Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu kutoka Omani Hemedi Bin Muhammed Al dhayan amesema lengo la ziara hiyo ni kuhakikisha Nchi mbili hizo zinakuwa karibu katika masuala mnali mbali hasa ya utamaduni na Historia.
Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na mambo ya Kale Fatma Mabrouk Khamisi amesema hatua hiyo itawasaidia kusoma kwa Histori hasa za Wafalme waliopita.