Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amepokea Salamu za Pole kwa Viongozi Wakuu na Viongozi Wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Viongozi wa Vyama vya siasa.
Waliotoa Salam za Pole ni Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dotto Mashaka Biteko, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah na baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi
Viongozi hao wameitaka Familia kuwa na subra katika kipindi hiki Kigumu cha Msiba wa kuondokewa na Mpendwa wao
Viongozi wengine walifuatana na Makamu wa Pili wa Rais ni pamoja Mhe.Haroun Ali Suleiman, Mhe.Tabia Maulid Mwita na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Leila Mohammed Mussa.
Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu Mhe. Mohamed Gharib Bilal nae amemfariji Dk.Mwinyi na Familia yake na kumuombea dua Marehemu Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mstaafu Balozi. Seif Ali Iddi na
Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa nao kwa Niaba ya Wananchi wa Mikoa Mitano ya Zanzibar na Wilaya zake wakawasilisha salamu za pole.
Aidha Dkt. Hussein Amepokea salamu za Pole kutoka kwa Vyama rafiki vya Siasa vilivyopo Nchini ambao nao wamemueleza Alhaj dk.Hussein kuwa Msiba huo ni wa wote.
Hayati Alhaji ali hassan Mwinyi Amefariki Dunia Februari 29 Jijini Dar Es Salaam na kuzikwa March Pili Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini, Unguja