Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameendelea kupokea salamu za pole kutoka kwa Viongozi Wastaafu, Serikali, Ndugu na Jamaa.
Hatua hiyo inafuatia Kifo cha Baba ake na Rais Mstaafu Marhum Hayati Ali Hassan Mwinyi.
Waliofika kutoa mkono wa pole ni Rais Mtaafu wa Awamu Saba Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, Spika wa Baraza la Wawakilish Mhe. Zubeir Ali Maulid, Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Ikulu Mhe.Ali Suleiman Mrembo, Mwakilishi wa Jimbo la Bubwini Mhe. Mtumwa Pea na Uongozi wa Chama Bubwini na Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Mstaafu Dkt. Abdulla Juma Sadalla Mabodi.
Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi Alifariki Dunia Tarehe, 29 Februari 2024, Dar es salaam na Kuzikwa Tarehe, 02 March 2024 huko Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja.