Watu Saba wamefariki Dunia na wengine 20 wanapatiwa Matibabu katika Hospitali ya Abdulla Mzee na Madaktari wanafanya Uchunguzi wa Ugonjwa usiojulikana.
Kufuatia tukio hilo Mganga Mkuu Wilaya ya Mkoani Dr. Haji Bakar Haji amesema tayari Madaktari wameanza uchunguzi kubaini chanzo na aina ya Ungonjwa atika Kisiwa hicho.
Akizungumza na Wananchi wa Kisiwa panza, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Rashid Abdalla Ali amewataka Wananchi kuwa waangalifu na Vyakula wanavyotumia hasa Wakati huu ambapo Serikali inafanya Uchunguzi.
Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Mtambile na Viongozi wengine wameshirikiana na Wananchi katika Msiba wa Watu Saba waliofariki katika Kijiji hicho.
stories
standard