Habari

JAMII IMETAKIWA KUISOMA ELIMU YA NDOA ILI KUISHI KATIKA MISINGI IMARA YA NDOA

Ukosefu wa Elimu ya Mafunzo ya Ndoa husababisha migogoro kwa wanandoa na kuvunjika kwa Ndoa hizo

Akizungumza katika Mahafali ya 21 ya Mafunzo ya Ndoa Mjumbe kutoka Baraza la Maulamaa Sheikh Suwedi Ali Suwedi amesema Ndoa inahitaji Elimu ili kujenga uvumilivu na upendo kwa Wanandoa.

Amesema Mafunzo hayo yatasaidia kupunguza engezeko kubwa la Talaka na Migogoro hivyo amewataka Wanafunzi hao kufuata nasaha walizopewa na Walimu ili kudumu katika Ndoa zao.

COCA-COLA YATOA MAFUNZO KWA WAJASIAMALI

    Kampuni ya Coca Cola imewataka Wajasiria Mali Wadogo  kutumia fursa zinazojitokeza na  kuwacha kuwa tegemezi katika Jamii .

    Akizungumza katika Mafunzo ya kuwajengea uwezo Wajasiria mali Wadogo wadogo wa Chakula Afisa Uhusiano wa Umma Mawasiliano na uendelevu Kampuni ya Coca Cola Ndg.Maria Kimwaga amesema lengo la Mafunzo haya ni kuwaelimisha Wanawake katika maswala ya Biashara pamoja na kuhakikisha wanajiwezesha Kiuchumi .

MWAMBA WA MAGEUZI WANANCHI WAMLILIA

    Wananchi wamesema  Tanzania imepoteza  Kiongozi  muhimu  katika Taifa Marehemu Ali Hassan Mwinyi ambae amejitoa  kuipigania Nchi ili kukuwa  na kusababisha kufunguka kiuchumi kupitia sera ya uwekezaji na kupiga hatua za maendeleo.

MUFTI WA ZANZIBAR AELEZA ALAMA ALIZOZIACHA MZEE MWINYI

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan ameshiriki kisomo cha Dua khitma alichokiandaa kwa ajili ya Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili Tanzania.

    Kisomo hicho kilichofanyika katika Viwanja vya Maonesho Nyamazi kimehudhuriwa na Viongozi na Wananchi mbalimbali.

RAISI SAMIA ATAKA TUYAISHI MAISHA YA MZEE MWINYI

    Mamia ya Wananchi na Viongozi mbali mbali wamejitokeza kuuaga Mwili wa Rais  Msaafu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Hayat  Ali Hassan Mwinyi .

 

    Ni Majira ya Saa Tatu Asubuhi Mmwili wa Hayat  Ali Hassan Mwinyi  uliondoshwa Kijijini kwake  Bweleo, baadhi ya Wananchi wa Kijiji hicho na wamemuelezea Kiongozi huyo alivyokuwa wakati wa uhai. 

MWISHO WA SAFARI YA MZEE MWINYI

    Mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Al-hajj Ali Hassan Mwinyi umezikwa leo katika Kijiji cha Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.

    Viongozi mbali mbali wa Kitaifa na Kimataifa wameshiriki Mazishi ya Marehem Ali Hassan Mwinyi pamoja na kutoa salamu zao za mwisho.

    Mapema Waumini na Viongozi hao walishiriki katika Sala ya Maiti katika Mskiti wa Jamil Zinjibar uliopo Mazizini Mkoa wa Mjini Magharibi

UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAAZI FUMBA KUANZA KARIBUNI

     Kampuni  ya Ishirini na Nne Kumi Clobal (2410) kutoka Uturuki inatarajia kuanzisha mradi wa ujenzi wa nyumba za maakazi ili jamii iweze kuishi  katika mazingira bora.

    Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti  wa mradi huo Tolga Tugtekin amesema  Nyumba hizo za kisasa zitakuwa katika maeneo ya Fumba ambapo Kampuni hiyo inafungua milango kwa Wananchi  kuweza kununua Nyumba hizo mradi utakapokamilika. 

WANANCHI WAELEZA JINSI WALIVYOMFAHAMU HAYATI MWINYI

     Baadhi ya Wananchi waeleza mazuri waliyoyafahamu na kuyajua kuhusu Hayati Mwinyi .

RIPOTI ZAELEZA KUWA UCHUMI WA TANZANIA UPO VIZURI

    Waziri wa Fedha SMT Dr. Mwigulu Nchemba amesema uchumi wa Tanzania umeendelea kuwa himilivu licha ya Dunia kukumbwa na misukosuko ya kiuchumi.

    D r. Mmwigulu Nchemba amesema hayo wakati wa majadiliano ya kimkakati ya ngazi ya juu yaliyofanyika Jijini Dar es salaam na kushirikisha Mawaziri, na Makatibu Wakuu wa SMT, SMZ, Mabalozi pamoja na Wadau wa maendeleo ambapo Waziri Mwigulu.

MAJALIWA AAGIZA UCHUNGUZI NDANI YA WIKI MOJA

    Waziri Mkuu  wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa ametoa Wiki moja kwa Taasisi ya Takukuru na Mkurungrzi wa Halmashauri ya Rorya kuhakikisha wanakamilisha uchunguzi wa wizi wa vifaa vya Skuli  uliofanywa na Mwalimu wa Skuli  ya Msingi Kinesi 'b' Wilayani Rorya.

    Kauli hiyo ameitoa katika mwendelezo wa Ziara yake Mkoa wa Mara Waziri Majaaliwa  ameagiza kukamika kwa uchunguzi huo ili kubaini ubadhilifu uliojitokeza katika Ujenzi wa Skuli hiyo ya Msingi Kinesi 'b'.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.