Habari

DKT. MWINYI AMEFARAJIKA NA JUMUIYA YA VETERAN YOUNG PIONEERS

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema amefarajika kuona Jumuiya Veteran Young Pioneers Zanzibar inapongeza utekelezaji mzuri wa ilani ya uchaguzi ya CCM katika kipindi cha Miaka Mitatu.

Akizungumza na Maveterani hao Ikulu Jijini Zanzibar amesema pongezi hizo zitakua chachu ya kuongeza kasi katika utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo.

Aidha Dkt. Mwinyi ameipongeza Jumuiya hiyo kwa kuendeleza Majukumu yao ya kujitolea, kuwafundisha Vijana Uzalendo, ukakamavu na itikadi ya Chama.

TIA INAANZA MFUMO MPYA WA KUSOMA KWA NJIA YA MTANDAONI

Taasisi ya Uhasibu Tanzania TIA inaanzisha Mfumo mpya wa kuwasaidia Wanafunzi kusoma Mtandaoni nje ya Vituo vyao vya Masomo.

Akizungumza katika Mafunzo kwa Wakufunzi wa Taasisi ya  uhasibu Tanzania (TIA), mratibu wa tathimini na ufuatiliaji Mradi wa HEET Magreth Emanuel amesema mradi huo umekusudia  kuwafikishia Wanafunzi masomo kupitia Mtandao kwenye maeneo yoyote watakayokuwepo.

WAANDISHI WA HABARI KUTUMIA KALAMU ZAO KULETA MABADILIKO

Waandishi wa Habari Nchini wameshauriwa kutumia Kalamu zao kuleta mabadiliko kwani Jamii inaamini kuwa Nguvu ya Kalamu zao inaweza kusaidia kujenga Taifa lenye kuzingatia Utu, Uadilifu, Amani na Utulivu.    

Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Latra Wakili Tumaini Silaa katika Semina ya kuwajengea uwezo Wanahabari Mabalozi iliyofanyika Kibaha Mkoani Pwani na kuongeza kuwa Mamlaka hiyo, imejipambanua kuheshimu na kutoa ushirikiano kwa Wanahabari Nchini.

WATENDAJI WIZARA YA MADINI KUFIKA TARIME VIJIJINI KUTATUA TATIZO LA FIDIA

Waziri Mkuu wa Tanzania amewagiza Watendaji wa Wizara ya Madini kufika Wilaya ya Tarime Vijijini  kuzungumza na Wananchi ili kutatua tatizo la fidia ambalo linawasumbua kwa muda mrefu na kuonekana wao Wakimbizi katika  ardhi yao.

Akizungumuza na Wananchi katika eneo la Nyamwaga baada ya kusikiliza  Kero hizo kutoka kwa  Wananchi waliokuwa wakizungumzia suala la fidia zinatolewa na Mgodi wa Barick North Mara.

MTAALA MPYA WA ELIMU UTAMFANYA MWANAFUNZI KUBADILIKA

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Lela Mohamed Mussa amesema Wizara ya Elimu kupitia Taasisi ya Elimu inafanya mabadiliko ya Mtaala mpya ili kuhakikisha unamjenga Mwanafunzi kuendana na mabadiliko hayo.

Akizungumza katika zoezi la uzinduzi wa ugawaji wa Vitabu vya Mtaala mpya Waziri Lela amesema kupitia Vitabu hivyo vitamjenga Mwanafunzi na mabadiliko ya kusoma kwa Vitendo na kujifunza ipasavyo hivyo amewataka Walimu kuvitumia Vitabu hivyo kwa kuvifundisha ipasavyo.

HALI YA UCHUMI ZANZIBAR KUKUA KWA ASILIMIA 7 NUKTA 2 KWA MWAKA 2024.

Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango imesema mwelekeo wa hali ya uchumi kwa Mwaka  2024 unakadiriwa kukua kwa wastani wa asilimia 7 nukta 2.

Dk Mkuya mapitio akiwasilisha Taarifa ya mapitio na mwelekeo wa mpango wa Maendeleo na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025. Waziri wa Wizara hiyo Dkt Saada Mkuya Salum amesema ukuwaji huo wa uchumi utatokana na kuendelea kuongezeka kwa uingiaji wa Watalii kwa Asilimia 30 .

WANANCHI JIMBO LA MTAMBILE WAPATIWA GESI BURE

    Wananchi wa Jimbo la Mtambile Wilaya ya Mkoani wametakiwa kuunga mkono juhudi za Serekali katika mapambano dhidi ya uharibifu wa mazingira kwa lengo la kuepuka athari za mabadiliko ya Tabianchi.

    Mbunge wa Jimbo la Mtambile Mhe.Seif Sloom sSeif ameyasema hayo katika hafla ya yakukabidhi majiko ya gesi kwa Wananchi Mia mbili Jimboni kwake, hafla hiyo iliyofanyika katika Banda la kununulia Karafuu lilipo Mtambile.

    Mara baada ya kukabidhiwa majiko hayo Masheha na Madiwani, wamewataka wanufaika wa msaada huo, kutumia kwa kuzingatia

KAMPUNI YA NOHA YAPELEKA FURAHA KWA HUYU MAMA

    Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee  na Watoto  Mhe.Riziki Pembe Juma amekabidhi Nyumba Mama wa Mtoto mwenye ulemavu mchanganyiko Abdilah Kassim, ili kumuondelea shida ya makazi  

KUTOKUWA WAKWELI KWA BAADHI YA MAWAKILI KUNAWACHAFULIA SIFA YAO

     Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla amewataka Mawakili wa Serikali na wa kujitegemea kushirikiana katika kutatua matatizo yanayowakabili ili kuhakikisha Wananchi wanapata haki bila upendeleo wowote.

     Ameeleza hayo wakati akifungua kikao cha Mawakili wa Serikali na Mawakili wa kujitegemea huko Tunguu kwa lengo la kujadiliana namna ya kuyatafutia ufumbuzi matatizo na kujadili mafanikio katika Mwaka mpya wa Sheria 2024.

JUKWAA LA KODI NA UWEKEZAJI KWA MWAKA 2024 LAZINDULIWA

    Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Philip Mpango amesema makusanyo ya Kodi Nchini Tanzania yamekua chini ya Asilimia 12 ya pato la Taifa kwa Takriban muongo mmoja sasa kiwango ambacho ni chini ya wastani wa asilimia 15.6 kwa Nchi za Bara la Afrika.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.