Habari

MAJAALIWA AWAPA MATUMAINI WANANCHI WALIOHAMISHWA ENEO LA NYANTWALI

     Waziri Mkuu wa Serekali ya Jamuhuri ya Muungano Mhe.Kassim Majaliwa amesema Serikali iko katika hatua za mwisho za kukamilisha utaratibu wa malipo ya Wananchi waliohamishwa eneo la Nyantwali ili kupisha hifadhi na Mapito ya Wanyama.

WAFANYABIASHARA WAMETAKIWA KUACHA KUPANDISHA BEI KIHOLELA

Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amewataka Wafanyabiashara kushirikiana na Serikali katika kuzingatia Bei za Bidhaa zao hasa katika Kipindi hiki cha kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza katika ziara ya kutembelea baadhi ya Masoko na Maeneo ya Biashara amesema Serikali itafanya kila iwezalo kuwasaidia Wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na kuwapunguzia ushuru kwa Bidhaa zinazotoka Nje ya Nchi ambazo ni muhimu ikiwemo Sukari ili kuhakikisha Wananchi wanamudu Maisha katika kipindi hicho.

TANZANIA KUANDIKA HISTORIA MATUMIZI YA TRENI YA UMEME

Kwa mara ya kwanza Tanzania imeandika Historia kupitia Shirika la Reli la Tanzania kwa kufanya majaribio ya kwanza ya kawaida ya Treni yake ya kisasa ya SGR inayotumia Umeme kutoka Dar Es Salaam hadi Mkoani Morogoro.

Treni hiyo ambayo ni ya kwanza kwa Afrika Mashariki inayotumia Umeme ambapo huduma Rasmi ya Safari zake zinatarajiwa kuanza Mwishoni mwa Mwezi wa Julai 2024.

ZANZIBAR NA SWEDEN ZIMEKUBALIANA KUIMARISHA SEKTA YA ELIMU

Serikali ya Mapinduzi ya zanzibar imetiliana   Saini ya makubaliano na Ubalozi wa Sweeden ili kusaidia kuimarisha Sekta ya Elimu Nchini.

Akizungumza katika hafla ya utiaji Saini huo katibu Mkuu Ofisi ya Raisi Fedha na Mipango Dkt Juma Malik Akili amesema lengo la makubaliano hayo ni kuanzisha mradi utakaosaidia kukuza Sekta ya Elimu kwa kuwajengea uwezo wa kufundisha Watendaji pamoja na kuimarisha Miundo mbinu ya Madarasa.

SMT NA SMZ ZIMEJIPANGA KUFANIKISHA MKUTANO WA WANACHAMA WA JUMUIA YA MADOLA

Wizara ya Katiba na Sheria ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimejipanga vyema katika kufanikisha Mkutano wa Mawaziri wa Sheria wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Madola.

KAMATI YABAINI UWEPO WA KASORO KWA BAADHI YA KANUNI

Kamati ya kanuni na Sheria ndogo ndogo ya Baraza La Wawakilishi imesema imebaini baadhi ya Kanuni kuwa na kasoro ikiwemo kuandikwa bila ya kuzingatia Vifungu wezeshi katika Sheria husika.

Akiwasilisha Ripoti ya Kamati Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Mihayo Juma N'hunga amezitaja kasoro nyengine ni baadhi ya Kanuni kuwasilishwa katika kamati bila kutangazwa katika Gazeti rasmi la Serikali jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

MHE. SHARIF, AMEWATAKA WATENDAJI KUWEKA KUMBUKUMBU

Waziri wa Afisi ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe Shariff Ali Shariff  amewataka Watendaji wa Taasisi hiyo kuweka kumbukumbu katika Utendaji wao wa kazi ili kuonesha hatua iliyofikiwa katika kazi zao.

Ameyasema hayo mara baada ya kukabidhiwa Afisi ya Rais, kazi Uchumi na Uwekezaji na aliyekuwa Waziri wa Afisi hiyo Mhe Mudrki Ramadhani soraga.

Mhe Shariff amewaomba Watendaji wa Ofisi hyo kuwa na ushirikiano katika kazi ili kuendeleza kazi nzuri wanazozifanya.

MAPINDUZI SEKTA YA AFYA YAFANYIKA JIMBO LA UZINI

    Jumla ya Ddola Laki Mmoja na Ishirini zimetumika kununulia vifaa vya Mmatibabu vitakavyotumika katika Hospitali Kkumi na Moja katika Jimbo la Uzini.

    Akikabidhi vifaa  hivyo  kwa Viongozi wa Jimbo la Uzini, Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Muzdalifa Ndg.Farouk Hamad ameiomba Serikali  kuendelea kuisaidia Jumuiya hiyo na kushirikiana nao, ili waweze kuleta misaada zaidi.

VIJANA WA CHUO WAPEWA ELIMU DAWA ZA KULEVYA

    Mamlaka ya Kkudhibiti na Kupambana na Dawa za Kkulevya Tanzania  DCEA imewataka Vijana wenye Umri wa Miaka 14 hadi 45, kujihadhari na matumizi ya Dawa za kulevya yanayoweza kuathiri Afya zao na kusababisha Taifa kupoteza nguvu kazi.

    Ushauri huo umetolewa Mwanza na Afisa wa Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa Ndg.Dezidel Tumbu wakati akitoa Elimu kuhusu Madhara ya Dawa za Kulevya kwa  Vijana  wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Tanzania Saut na Chuo cha Afya City College Wilaya wa Magu.

MASHEIKH ,WANAZUONI , NA MAMUFTI AFRIKA WAOMBEWA DUA

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema ustawi wa maisha umechangiwa na kazi kubwa walioifanya Masheikh pamoja na Waalimu wa Dini waliotangulia mbele ya haki.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.