WAFANYABIASHARA WAMETAKIWA KUACHA KUPANDISHA BEI KIHOLELA

RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amewataka Wafanyabiashara kushirikiana na Serikali katika kuzingatia Bei za Bidhaa zao hasa katika Kipindi hiki cha kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza katika ziara ya kutembelea baadhi ya Masoko na Maeneo ya Biashara amesema Serikali itafanya kila iwezalo kuwasaidia Wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na kuwapunguzia ushuru kwa Bidhaa zinazotoka Nje ya Nchi ambazo ni muhimu ikiwemo Sukari ili kuhakikisha Wananchi wanamudu Maisha katika kipindi hicho.

Aidha Dkt Mwinyi amewasisitiza Wafanyabiashara kutotumia kipindi hicho cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kupandisha Bei bila ya sababu na kuutaka uongozi wa Masoko kusimamia suala la upandaji wa Bei holela.

Nao baadhi ya Wananchi wamesema hivi sasa Mfumuko wa Bei ni mkubwa na wanaelekea katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hivyo ni vyema Serikali kuliangalia jambo hilo ili Wafanyabiashara na wananchi waweze kufaidika.

Nao Wafanyabiashara hao wamemuhakikishia Dkt. Mwinyi kuwa hawatopandisha Bei bila ya sababu za msingi huku wakiomba kuendelezwa kwa mnada katika Soko la Jumbi, pamoja na kupatiwa Mikopo ili kuimarisha Bishara zao. 

Maeneo aliyoyatembelea Raisi Dk Mwinyi ni pamoja na Soko la Mnada wa Vyakula Jumbi, Soko la Samaki Malindi, Bandari ya Malindi pamoja na Soko la Darajani.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.