Habari

WAFANYAKAZI ZBC WAPATA MAFUNZO YA MPANGO MKAKATI WA SHIRIKA

    Afisa Utawala wa Shirika la Utangazaji Zanziabr ZBC Ndg.Salum Jecha amesema Shirika hilo limejipanga kuimarisha vipindi vyake vya  matangazo ya Redio na televisheni  katika Mikoa yote yaTanzania ili kuendeana na kasi ya mabadiliko ya Dunia.

    Akizungumza mara baada ya kumalizika Mafunzo ya Wafanyakazi wa ZBC Afisa huyo amesema  ZBC itahakikisha inatumia rasilimali zake ili kuendana na kasi ya Dunia katika Tathnia ya habari kwa kutoa  Mafunzo kwa Wafanyakazi wa Shirika hilo ili kuendana na Teknolojia ya Habari.

UNICEF YASAIDIA SEKTA ZA AFYA, ELIMU NA WATOTO ZANZIBAR

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman amesema Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto Duniani  (UNICEF) limekuwa na msaada kwa Zanzibar katika Sekta mbalimbali ikiwemo ya Afya, Elimu pamoja na haki za Watoto.

TAZAMA JINSI WAZIRI SHARIF ALIVYOKULA KIAPO

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemuapisha Mhe. Shariff Ali Shariff ambae ni Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi Uchumi na Uwekezaji.

    Hafla ya Uapisho huo umefanyika Ikulu Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi, Viongozi wa Kisiasa, Uongozi wa Wizara ya Kazi Uchumi na Uwekezaji pamoja na Familia.

    Mhe.Shariff Ali Shariff anashika dhamana ya Wizara hiyo kufuatia mabadiliko madogo aliyoyafanya hivi karibuni.

 

FURSA ZA UWEKEZAJI ZAFUNGUKA ZIARA DKT.SAMIA

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Raisi, (Uwekezaji) Profesa Kitila Mkumbo amesema mbali na kukuza uhusiano wa kidiplomasia na kisiasa ziara za Raisi Samia katika Mataifa mbalimbali zina faida nyingi zikiwemo za ukuzaji wa uchumi.

SERIKALI KUENDELEA KUJENGA MIUNDOMBINU KATIKA MAENEO YA UTALII

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Hussein Ali Mwinyi  amesema Serikali itaendela kujenga Miundombinu  katika maeneo ya Utalii  ili Wananchi waweze  kufanya shughuli zao kwa  uhakika.

Akifungua Mkutano wa pili wa Wadau wanaouza Bidhaa za Utalii kutoka Nchi mbali mbali Duniani, huko Golden Tulip Uwanja wa Ndege,amesema Miundo Mbinu hiyo itaongeza ukuaji wa Uchumi na pato la Taifa.

WAKANDARASI WAMEHIMIZWA KUKAMILISHA KWA WAKATI MADUKA DARAJANI SOUK

Waziri wa Nchi afisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ, Mhe Masoud Ali Mohammed, amewataka Wakandarasi wa Ujenzi wa Maduka ya Darajani, kulifanya eneo hilo kuwa kivutio kwa Watumiaji. 

 Akikagua Ujenzi wa Maduka unaoendelea  wa Awamu ya Pili wa Darajani Souk, unaejengwa na Kampuni ya Simba Developers,  amewataka kuhakikisha kuwa Ujenzi huo unakamilika kwa wakati na ubora ili kuweka Mji katika Mazingira mazuri.

VETA NA KIST ZAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe Leila Mohamed Mussa amesema Serikali imekusudia kuzalisha Walimu wenye viwango kupitia ufundi na Mafunzo ya Amali. 

Waziri Lela ametoa Kauli hiyo, katika utiaji Saini kati ya Taasisi ya Sayansi na Ufundi (KARUME) na Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA) kwa lengo la kukuza na kuzalisha Walimu wapya wenye uwezo wa kufundisha ufundi na Mafuzo ya Amali.

Mh: Lela amezipongeza Taasisi zote mbili na amesema hatua hiyo itasaidia kukuza umoja na ushirikiano kati ya Bara na Visiwani.

MRADI WA KIDIGITALI KUIMARISHA ZAIDI MAWASILIANO

Katika kuimarisha mradi wa Tanzania ya Kidigitali Serikali zote mbili zimeamua kuwa na mfumo wa pamoja  ili kuimaraisha taarifa muhimu zikiwemo za watu Binafsi.

Akizungumza katika Mkutano wa pamoja wa kuutambulisha Mradi huo kwa Watendaji wa Bara na Zanzibar katibu Mkuu Wizara ya habari Mawasiliano na Teknolojia Mohammed Khamis Abdallah amesema hatua hiyo itasaidia matumizi salama ya mawasiliano

WALIMU WA MADRASA KUZINGATIA UADILIFU

Waziri wa Nchi ofisi ya  Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala bora Mhe Harouna Ali Suleiman amezitaka Madrasa za Dini kusimamia misingi ya Kiislam ili kutokomeza vizendo vya uhalifu.

Akifunga Mafunzo ya Walimu wa Madrasa ya Elimu ya Amali Waziri Haroun amesema misingi   ya Dini iliyobora humjenga Mwanafunzi kuwa na Muongozo mwema katika Uislamu hivyo ni vyema kuhakikisha Mafunzo hayo yanaleta tija kwa Walimu.

KAMATI BLW HAIRIDHISHWI NA JENGO LA BARAZA LA MITIHANI.

Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wakilishi imesema hairidhishwi na Mazingira ya Jengo la Ofisi za Baraza la Mitihani

Kutokana na umuhimu wake na hali iliokuwa nayo.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.