Waziri wa Nchi, Ofisi ya Raisi, (Uwekezaji) Profesa Kitila Mkumbo amesema mbali na kukuza uhusiano wa kidiplomasia na kisiasa ziara za Raisi Samia katika Mataifa mbalimbali zina faida nyingi zikiwemo za ukuzaji wa uchumi.
Akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari Ikulu Jijini Dar es salaam Profesa Kitila Mkumbo amesema miongoni mwa faida hizo ni uwekezaji unaoendelea kufanyika wa Ujenzi wa Viwanda mbalimbali hapa Nchini ikiwemo Kiwanda cha kisasa cha kutengeneza vioo (Sapphire Glass ltd) kilichopo, Wilaya ya Mkuranga ambacho ni matokeo ya ziara ya Raisi Nchini China.
Prof. Mkumbo amesitiza kuwa uwekezaji ni mchakato ambao una hatua kadhaa, hivyo matokeo ya ziara za Rais Samia yanajidhihirisha kupitia Sekta mbalimbali.
Akizungumzia suala la usalama wa Chakula na Kilimo ambalo ni moja ya Sekta zilizosainiwa mikataba katika ziara ya Rais Samia Nchini Norway Waziri wa Kilimo Hussen Bashe .
Ameongeza kuwa Serikali ya Tanzania imeamua kuandaa utaratibu wa matumizi ya fedha za Wafadhili katika kutatua changamoto za msingi ikiwemo ufanyaji wa tafiti hususan za Afya ya udongo.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Shaibu Saidi Mussa akatolea ufafanunuzi suala laSanamu la Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere iliyozinduliwa hivi karibuni Addiss Ababa Etheopia.
Awali Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunnus alieleza mafanikio ya ziara za Rais Samia Nchini Norway, Vatican na Ethiopia.