Katika kuimarisha mradi wa Tanzania ya Kidigitali Serikali zote mbili zimeamua kuwa na mfumo wa pamoja ili kuimaraisha taarifa muhimu zikiwemo za watu Binafsi.
Akizungumza katika Mkutano wa pamoja wa kuutambulisha Mradi huo kwa Watendaji wa Bara na Zanzibar katibu Mkuu Wizara ya habari Mawasiliano na Teknolojia Mohammed Khamis Abdallah amesema hatua hiyo itasaidia matumizi salama ya mawasiliano
Amesema hatua hiyo ni sehemu ya uimarishaji mawasiliano na kuchochea matumizi ya Tehama pamoja na mkakati wa kukuza uchumi wa Kidigitali.
Katibu Mkuu Wizara ya ujenzi Mawasiliano na uchukuzi Khadija Khamis Rajab amesema kupitia Mradi huo Zanzibar itaweza kunufaika kwa kutanua mawasiliano ikiwemo uongezaji wa Minara ambayo kwa sasa haitoshelezi.
Kiongozi wa Timu ya Wataalamu wa Benki ya Dunia Paul Seanen amesema lengo lao ni kuona wanaimarisha maisha bora kwa Wananchi hasa katika kutengeneza ushirikiano kati ya Serikali na Taasisi Binafsi
Mradi wa Tanzania ya Kidijitali unaofadhiliwa na Benki ya Dunia unatarajiwa kumalizika 2026 ambapo jumla ya Dola Milioni 150 zitatumika.