Habari

KIWANDA CHA KUCHAKATA MWANI CHAMANANGWE MBIONI KUKAMILIKA

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi Zanzibar iko tayari kushirikiana na Nutri-Sun Limited kutoka Uingereza katika kukamilisha mradi wa Kiwanda cha kuchakata Mwani kilichopo Chamanangwe, Pemba.

    Akizungumza na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania David Conar na Ujumbe wake Ikulu Zanzibar Raisi Dk. Mwinyi amesema hatua ya kukamilika Kiwanda hicho kitarahisisha kupata Soko la uhakika kwa Wakulima wa zao hilo na kuwaenua Kiuchumi.

RC MJINI ASISITIZA AMANI NA USHIRIKIANO BAINA YA DINI TOFAUTI

    Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe.Idrissa Kitwana Mustafa amesema Serikali itahakikisha Wananchi wa Mkoa huo wanaendelea kuishi pamoja licha ya tofauti zao za imani ya Dini.

WALIOJENGA NDANI YA HIFADHI YA BARABARA SHERIA ZITAWAHUKUMU

    Wakala wa Barabara Zanzibar umewasisitiza Wananchi kuacha tabia ya kujenga kiholela  ndani ya hifadhi ya Barabara ili kuepuka usumbufu utakaoweza kutokea.

WATENDAJI SERIKALI ZA MITAA WATAKIWA KUACHA MIVUTANO

     Watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wametakiwa kuacha mivutano isiyo na msingi na badala yake washughulikie utekelezaji wa kazi za maendeleo ya Wananchi.

     Akizungumza na Wakurugenzi, Mameya na Wenyeviti wa Kamati za Madiwani, Makao Makuu ya Kikosi cha Valantia Mtoni, Waziri wa Nchi Ofisi ya RaisTawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Masoud Ali Mohammed, amesema mivutano baina yao imekuwa ikizorotesha upatikanaji huduma muhimu kwa Wananchi.

KMKM YANASA SIMU MAFUTA SABUNI NA NYAVU KIMAGENDO

     Kikosi cha kuzuia Magendo KMKM kimeokota Marobota 4 yenye  Box 16 za Simu Aina ya Infinix 40 lililokuwa linataka kusafirishwa kwa njia ya Magendo katika Bandari zisizi rasmini  Chuini  Masinde.

    Akizungumza Eneo la Kama Msaidizi Mkuu wa Kamandi Kaskazini LCDR Idrisa Hamdani  na Mkuu wa Operesheni Kamandi ya Kaskazini LCDR Rashid Masemo  wamesema  katika Doria  ya kawaida wamekuta Marobota  4 ya simu  wakiwa katika harakati za kusafirishwa mzigo huo ambapo Wahusika wamekimbia na kuuwacha mzigo huo.

CHIMBO JIPYA LA MCHANGA LAFUNGULIWA

      Wizara ya Nishati na Madini imewasisitiza Wafanyabiashara wa mchanga kuacha tabia ya kuweka Soko la Mchanga na Maliasili nyengine katika eneo la Taveta.

    Akitoa Taarifa ya Ufunguzi wa shimo la mchanga kwa matumizi ya miradi Zanzibar Waziri wa Maji Nishati na Madini Mhe. Shaibu Hassan Kaduara amesema eneo la Taveta ni sehemu ambayo imepita line kubwa ya Umeme hivyo kuendelea kufanya Biashara katika eneo hilo ni kuhatarisha usalama wao .

RAIS MWINYI AFUNGUA MKUTANO MKUU ZNCC

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka Wafanyabiashara kuendesha biashara zao kwa kuzingatia misingi ya haki na uadilifu na kulipa kodi ili Serikali iweze kukusanya Mapato na kuendelea kutoa huduma bora kwa Jamii.

ZSTC KUNUNUA SUKARI YOTE KATIKA KIWANDA CHA MAHONDA

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Shirika la Biashara la Taifa imesema itainunua Sukari yote katika Kiwanda cha uzalishaji Sukari Mahonda na kupunguza Bei ya Bidhaa hiyo ili Wananchi waweze kumudu Gharama zake hasa katika Kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

SMZ IMETENGA FEDHA KUJENGA UPYA DAHALIA YA SKULI YA UFUNDI KENGEJA

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa amewataka Wanafunzi wa Skuli ya Ufundi Kengeja kuitunza na kulinda vyema Miundo mbinu ya Skuli hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu.

Akikabidhi Eneo la Ujenzi wa Daghalia kwa Kampuni ya Ujenzi ya United Ramp kufuatia kuungua Moto kwa Bweni la Wanaume la Skuli hiyo Waziri lela amesema Serikali kupitia Wizara ya Elimu imetenga Fedha kwa ajili ya kujenga upya Daghalia hiyo hivyo amewataka Wanafinzi hao kuthamini Miundo mbinu hiyo kwa Maslahi yao na Vizazi vijavyo.

SMT KUIMARISHA MIFUMO YA UOKOAJI ILI KUPUNGUZA VIFO MWANZA

Wakazi wa Mkoa wa Mwanza wameiomba Serikali kuimarisha Mifumo ya Uokoaji inayotumiwa na Jeshi la Zimamoto na uokoaji ili kupunguza Vifo vitokanavyo na Majanga ya Watu kuzama Maji yanayotokea katika Ziwa Victoria.

Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Mwanza wameyasema hayo wakati Jeshi la Zimamoto na uokoaji likitoa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Wavuvi katika kukabiliana na Majanga ya Moto ndani ya Maji.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.