Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa amewataka Wanafunzi wa Skuli ya Ufundi Kengeja kuitunza na kulinda vyema Miundo mbinu ya Skuli hiyo ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
Akikabidhi Eneo la Ujenzi wa Daghalia kwa Kampuni ya Ujenzi ya United Ramp kufuatia kuungua Moto kwa Bweni la Wanaume la Skuli hiyo Waziri lela amesema Serikali kupitia Wizara ya Elimu imetenga Fedha kwa ajili ya kujenga upya Daghalia hiyo hivyo amewataka Wanafinzi hao kuthamini Miundo mbinu hiyo kwa Maslahi yao na Vizazi vijavyo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mwanakhamis Adam Ameir amewataka Wanafunzi wa Skuli hiyo kuwa na Tabia ya kukagua Umeme kabla ya kulala au kutoka kwa lengo la kuweka tahadhari na matukio ya Moto.
Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mwalimu Muh’d Nassor Salim amewataka Wanafunzi kuhakikisha wanaongeza bidii katika Masomo yao ili kupata Wataalamu watakao isaidia Serikali hapo baadae.