KMKM YANASA SIMU MAFUTA SABUNI NA NYAVU KIMAGENDO

Kuzuia magendo

     Kikosi cha kuzuia Magendo KMKM kimeokota Marobota 4 yenye  Box 16 za Simu Aina ya Infinix 40 lililokuwa linataka kusafirishwa kwa njia ya Magendo katika Bandari zisizi rasmini  Chuini  Masinde.

    Akizungumza Eneo la Kama Msaidizi Mkuu wa Kamandi Kaskazini LCDR Idrisa Hamdani  na Mkuu wa Operesheni Kamandi ya Kaskazini LCDR Rashid Masemo  wamesema  katika Doria  ya kawaida wamekuta Marobota  4 ya simu  wakiwa katika harakati za kusafirishwa mzigo huo ambapo Wahusika wamekimbia na kuuwacha mzigo huo.

    Wakati huohuo katika Eneo la Chumbe Mnarani Kikosi hicho kimekamata  Mashua yenye  bidhaa mbali mbali ikiwemo  Mafuta ya kupikia zaidi ya Dumu Mia Tatu, Sabuni Polo 3 Mifuko na Robota Moja la Nyavu za kuvulia  bila kibali chochote  zipelekea Dar es salaam.

    Msaidizi Mkuu wa Kamandi ya Kusini Kamanda Ndg.Bakari Salum Othman na Mkuu wa Operesheni Kamandi ya Kusini Ndg. Ali Omar Ali ameziomba Taasisi husika kuongeza ushirikiano ili kupambana na Vitendo vya usafirishaji wa  mali za Magendo.

    Nahodha wa Mashua hiyo Ndg. Shaibu Khamis Faki amekiri kukutwa na mali ya Magendo bila ya Vitambulisho vyovyote vya uthibitisho wa bidhaa alizozibeba.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.