Wakala wa Barabara Zanzibar umewasisitiza Wananchi kuacha tabia ya kujenga kiholela ndani ya hifadhi ya Barabara ili kuepuka usumbufu utakaoweza kutokea.
Akizungumza wakati wa utiaji alama nyekundu huko Paje, Jambiani na Makunduchi kwa waliojenga Maduka, Mabanda ya Biashara na Majengo mengine ndani ya miundo mbinu ya Barabara msimamizi wa Kitengo cha Ujenzi Wakala wa Barabara Zanzibar Ndg. Omar Mohammed Ngomambo amesema wamekuwa wakiwapa tahadhari Wananchi ili waweze kutambua kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Afisa Kitengo cha Uhusiano Wakala wa Barabara Ndg.Mulhati Hassan Ally ametoa wito kwa Wananchi kuacha tabia kujenga karibu na hifadhi ya Barabara. Kazi hiyo inatarajiwa kufikia asilimia mia moja kwa Unguja na Pemba.