Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi Zanzibar iko tayari kushirikiana na Nutri-Sun Limited kutoka Uingereza katika kukamilisha mradi wa Kiwanda cha kuchakata Mwani kilichopo Chamanangwe, Pemba.
Akizungumza na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania David Conar na Ujumbe wake Ikulu Zanzibar Raisi Dk. Mwinyi amesema hatua ya kukamilika Kiwanda hicho kitarahisisha kupata Soko la uhakika kwa Wakulima wa zao hilo na kuwaenua Kiuchumi.
Balozi wa Uingereza Nchini David Conar amemweleza Rais amesema Mipango ya kupata Mashine na Teknolojia ya kuchakata Mwani imekamilika hivyo ifikapo Mwishoni mwa Mwaka 2024 Kiwanda hicho kitaanza kuzalisha kazi.
Marisa Drew kutoka Benki ya Standard Chartered amemhakikishia Rais Dk. Mwinyi upatikanaji endelevu wa fedha ambazo zitatumika kununulia Mashine na zao la Mwani, na kueleza kuwa Kiwanda hicho kitawawezesha Wakulima wa Mwani hasa Wanawake na Vijana kujikwamua Kiuchumi.