ZSTC KUNUNUA SUKARI YOTE KATIKA KIWANDA CHA MAHONDA

WAZIRI WA BIASHARA, MAENDELEO YA VIWANDA

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Shirika la Biashara la Taifa imesema itainunua Sukari yote katika Kiwanda cha uzalishaji Sukari Mahonda na kupunguza Bei ya Bidhaa hiyo ili Wananchi waweze kumudu Gharama zake hasa katika Kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kauli hiyo ameitoa na Waziri wa Biashara, Maendeleo ya Viwanda Mhe Omar Said Shabaan wakati alipofanya ziara katika Kiwanda hicho amesema ni jukumu la Serikali kuhakikisha inawaondolea usumbufu Wananchi wake hivyo imeona ipo haja ya kununua Bidhaa hiyo ili kupatikana kwa Bei inayopangwa na Serikali.

Aidha ameupongeza uongozi wa Kiwanda hicho kuendelea kuthamini na kuunga Mkono juhudi za Serikali kwa kuzalisha Bidhaa hiyo kwa wingi.

Meneja wa Rasili mali Watu katika Kiwanda cha Sukari Mahonda Bashiri Waziri Mohamed amesema matarajio yao ni kuzalisha Tani Elfu Tano ili kuwasaidia Wananchi kuondokana na tatizo la upungufu wa Bidhaa hiyo hasa katika kipindi cha mfungo wa Ramadhan.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.