Wizara ya Nishati na Madini imewasisitiza Wafanyabiashara wa mchanga kuacha tabia ya kuweka Soko la Mchanga na Maliasili nyengine katika eneo la Taveta.
Akitoa Taarifa ya Ufunguzi wa shimo la mchanga kwa matumizi ya miradi Zanzibar Waziri wa Maji Nishati na Madini Mhe. Shaibu Hassan Kaduara amesema eneo la Taveta ni sehemu ambayo imepita line kubwa ya Umeme hivyo kuendelea kufanya Biashara katika eneo hilo ni kuhatarisha usalama wao .
Kaduara katika Ufunguzi huo amesema Wizara haijafanya mabadiliko yoyote ya Bei za maliasili zisizorejesheka na kuwataka Madereva kuacha tabia ya kusingizia ugumu wa upatikanaji wa vibali na kuwalaghai Wananchi.
Wizara ya, Maji Nishati na Madini imefungua eneo jipya la kuchimba Mchanga ambalo linamilikiwa na Ndg. Hamad Omar lilipo Shehia ya Donge Mchangani Wilaya ya Kaskazini 'a' kwa ajili ya matumizi ya Miradi .