WATENDAJI SERIKALI ZA MITAA WATAKIWA KUACHA MIVUTANO

Watendaji serikali za mitaa

     Watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wametakiwa kuacha mivutano isiyo na msingi na badala yake washughulikie utekelezaji wa kazi za maendeleo ya Wananchi.

     Akizungumza na Wakurugenzi, Mameya na Wenyeviti wa Kamati za Madiwani, Makao Makuu ya Kikosi cha Valantia Mtoni, Waziri wa Nchi Ofisi ya RaisTawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Masoud Ali Mohammed, amesema mivutano baina yao imekuwa ikizorotesha upatikanaji huduma muhimu kwa Wananchi.

    Amesema Watendaji wa Mabaraza ya Manispaa, Mabaraza ya Mji na Halmashauri, Wanajukumu la kuandaa mipango ya miradi ambayo itaendana na mahitajio ya Wananchi ili iweze kuwanufaisha.

    Mkurugenzi mipango Sera na Uratibu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ, Ndg. Abdallah Issa mgongo, amezitaka Serikali za Mitaa kuandaa mapema Bajeti zenye maslahi na walengwa ili ziweze kuuganishwa katika Bajeti ipate kusomeka Kitaifa. 

    Nao Mkurugenzi wa Baraza la Mji Mkoani Ndg. Yussuf Kaiza Makame na Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Kusini Unguja, Mustafa Mohammed Haji, wamesema wataendeleza ushirikiano  katika kuandaa mipango yenye tija na Wananchi ili kuleta ufanisi na kufikia malengo yaliyokusudiwa.  

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.