SMT KUIMARISHA MIFUMO YA UOKOAJI ILI KUPUNGUZA VIFO MWANZA

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

Wakazi wa Mkoa wa Mwanza wameiomba Serikali kuimarisha Mifumo ya Uokoaji inayotumiwa na Jeshi la Zimamoto na uokoaji ili kupunguza Vifo vitokanavyo na Majanga ya Watu kuzama Maji yanayotokea katika Ziwa Victoria.

Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Mwanza wameyasema hayo wakati Jeshi la Zimamoto na uokoaji likitoa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Wavuvi katika kukabiliana na Majanga ya Moto ndani ya Maji.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji Mkoa wa Mwanza Kamila Labani amesema Elimu ya namna ya kukabiliana na Majanga ya Moto Majini imeshatolewa kwa Wavuvi waliopo katika baadhi ya Visiwa vya Wilaya za Muleba, Sengerema na Ukerewe.

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala amesema Elimu hiyo itasaidia kuwaandaa Watu kujiokoa kutokana na Ziwa Victoria kuwa na shughuli nyingi za kiuchumi, huku Mkurungenzi wa Manispaa ya Ilemela kiomoni Kibamba akiwataka Wafanyabiashara kuweka Vifaa vya kuzimia Moto katika Biashara zao.

Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Mkoa wa Mwanza Pius Kambanga ameipongeza Serikali kwa kueendelea kuimarisha shughuli za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kuweka Mifumo na kununua Vifaa vya kisasa yakiwemo magari.

Kazi hiyo imeendeshwa kwa ushirikiano wa Jeshi la Zimamoto na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.