Habari

WAJUMBE BLW WASIKITISHWA NA BEI ZA BIDHAA KUPANDA KIHOLELA

Kamati ya Utalii Biashara na Kilimo imesema imesikitishwa na kitendo cha Mamlaka za Serikali za Mitaa kushindwa kutekeleza matakwa ya Kisheria ya kuipatia Wakala wa Uwezeshaji Kiuchumi asilimia 10 ya Pato la ndani linalokusanywa na Mamlaka hizo.

Akiwasilisha Ripoti ya Kamati hiyo Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Mtumwa Pea Yussuph amesema hali hiyo inapelekea maombi mengi kutoka kwa makundi hayo kukosa mikopo kutokana. na. Uhaba wa Fedha.

WANANCHI KISHAPU WAJAA HOFU BAADA YA ZIARA YA MAKONDA

    Baadhi ya Wakazi wa Vijiji 11 vinavyozunguka Mgodi wa Mwekezaji El-hillal uliopo Mwadui Wilayani Kishapu wameingiwa na hofu ya kukamatwa na Vyombo vya Dola baada ya kutoa malalamiko yao mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Mheshimiwa Paul Makonda.

    Wananchi hao wamesema hofu yao inatokana na Maofisa Uhamiaji Mkoani Shinyanga kufika Kijijini kwao wakimtafuta Mwanakijiji Mwenzao Ndg. Juma Kapina ambaye walikwenda kufanya naye Mahojiano.

WATERFALL CHARITY YATOA MSAADA WA VYAKULA PEMBA

      Wananchi wa Shehia ya Makombeni Wilaya ya Mkoani wameishukuru Taasisi ya Waterfall Charity kwa kuwapatia msaada wa Vyakula mbalimbali kwa ajii ya maandalizi ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.Shukrani hizo zimetolewa mara baada ya kupokea msaada huo huko Kiwanja cha Mpira wa miguu Makombeni.

WAZIRI UCHUMI WA BULUU AKAGUA KIWANDA CHA KUSARIFU DAGAA - KAMA

    Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe.Shaabani Ali Othman amemtaka Mkandarasi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Kusarifu Dagaa Kama kumaliza ujenzi kwa wakati ili kuwapa nafasi Wajasriamali kuendelea na shughuli za ukaushaji Dagaa.

     Waziri Shaaban amesema hayo huko Kama Wilaya ya Magharib 'a' baada ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Kiwanda hicho.amesema Serikali imedhamiria kuweka mazingira bora ya Wajasriamali wakiwemo Waanika Dagaa hivyo amemtaka Mkandarasi huyo kuhakikisha anamaliza Ujenzi huo ifikapo Agosti Mwaka huu.

DC KUSINI UNGUJA AHAMASISHA USAFI WA FUKWE

    Mkuu wa Wilaya ya Kusini Galos Nyimbo amewahimiza Wananchi kuendelea kuweka Mji katika hali ya usafi kufanya hivyo utaongeza idadi ya Watalii kuitembelea Zanzibar.

     Akizungumza katika usafi wa mazingira huko Michamvi ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Familia ya Polisi .  Polisi  Familly Day amesema Jeshi la Polisi ni Sehemu ya Jamii, hivyo kufanya usafi itaishajihisha Jamii kuhifadhi na kutunza Mazingira ambayo ni miongoni mwa vivutio vya Wageni katika Fukwe.

BEN-BELLA YAADHIMISHA MIAKA MIA YA KUANZISHWA KWAKE

      Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimesema zitaendelea kuipa kipaumbele Sekta ya Elimu ili Wanafunzi wapate Elimu iliyo bora.

    Akimwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Katika maadhimisho ya Miaka 100 ya kuazishwa kwa Skuli ya Benbella, huko Uwanja wa Mnazi Mmoja, Waziri wa Maendeleo ya Jamaii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Riziki Pembe Juma, Amesema Sekta ya Elimu inamchango mkubwa wa kuleta mageuzi Nchini.

WANAFUNZI GEITA WALIA NA HUDUMA YA VYOO

    Zaidi ya Wanafunzi 1500, wa Shule ya Msingi Ludeba katika Kijiji cha Ludeba, Kata ya Ipalamasa, Wilaya ya Chato Geita wanakabiliwa na  ukosefu wa Vyoo vya kisasa hali inayosababisha  taaluma kushuka.
   Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhandisi Deusdedith Katwale amewashauri Wananchi wa Kata ya Ipalamasa  kuhakikisha anasimamia upatikanaji wa huduma muhimu katika Shule ya Msingi Ludeba na Serikali inaendelea kuimarisha miundo mbinu ya huduma za Kijamii.

MWAKILISHI AIMWAGIA SIFA ZBC

  Mwakilishi wa jimbo la Kikwajuni Mhe. Nassor Salim Jazira alipongeza Shirka la Utangazaji Zanzibar ( ZBC) kwa kitendo chake cha kutangaza kutoa huduma ya Matangazo ya vifo bure bila ya gharama yeyote kwa kipindi chote cha mfungo wa mwezi mtuku wa Ramadhani.

  Sifa hizo amezitoa leo katika ukumbi wa Baraza la wawakilishi  huko Chukwani wakati wa kikao kikiendelea.

STASHAHADA ZILIZOPEWA KIPAUMBELE KUPATIWA MKOPO

    Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali inakusudia kuanzisha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu yenye lengo la kutoa fursa za Mikopo kwa Wanafunzi wa Kizanzibari wenye sifa za kujiunga na Masomo Ngazi mbali mbali za Elimu ya juu Ndani na Nje ya Nchi.

ORODHA YA WAPIGA KURA WAPYA KUWEKWA WAZI

   Tume ya Uchaguzi Zanzibar imetangaza kuweka wazi Orodha ya Wapiga Kura Wapya katika Vituo vilivyotumika uandikishaji kwa Unguja na Pemba kwa muda wa Siku Saba.

    Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji George Joseph Kazi ameyasema hayo katika Ukumbi wa Sheikh Idris Abdulwakil Kikwajuni kwa Wadau wa Uchaguzi kuhusu uandukishaji wa Wapiga Kura Wapya na uwekaji wazi Orodha za Wapiga Kura .

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.