Baadhi ya Wakazi wa Vijiji 11 vinavyozunguka Mgodi wa Mwekezaji El-hillal uliopo Mwadui Wilayani Kishapu wameingiwa na hofu ya kukamatwa na Vyombo vya Dola baada ya kutoa malalamiko yao mbele ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa Mheshimiwa Paul Makonda.
Wananchi hao wamesema hofu yao inatokana na Maofisa Uhamiaji Mkoani Shinyanga kufika Kijijini kwao wakimtafuta Mwanakijiji Mwenzao Ndg. Juma Kapina ambaye walikwenda kufanya naye Mahojiano.
Ndg. Juma Kapina na Mwenzake Ndg.Ally Kagoo hapa wanafafanua kuhusiana na tukio hilo huku Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Masagala akithibitisha kuwapokea Maofisa Uhamiaji Ofisini kwake.
Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Shinyanga Ndg.Emmanuel Kajura kwa sharti la kutopigwa picha amekiri kuhojiwa kwa Mwananchi huyo na kwamba mahojiano hayo ni moja ya utaratibu wa kawaida wa Ofisi yake.