Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe.Shaabani Ali Othman amemtaka Mkandarasi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Kusarifu Dagaa Kama kumaliza ujenzi kwa wakati ili kuwapa nafasi Wajasriamali kuendelea na shughuli za ukaushaji Dagaa.
Waziri Shaaban amesema hayo huko Kama Wilaya ya Magharib 'a' baada ya kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Kiwanda hicho.amesema Serikali imedhamiria kuweka mazingira bora ya Wajasriamali wakiwemo Waanika Dagaa hivyo amemtaka Mkandarasi huyo kuhakikisha anamaliza Ujenzi huo ifikapo Agosti Mwaka huu.
Mkuu wa Jeshi la kujenga Uchumi Zanzibar JKU Kanal Haji ameithibitishia Serikali kuwa Ujenzi utakamilika kwa wakati endapo atakamilishiwa fedha zilizobakia.
Mwenyekiti wa Kamati ya Waanika Dagaa Kama Ndg.Khamis Khamis Vuai ameishukuru Serikali kuwapatia eneo hilo kwa ajili ya kuanikia Dagaa
Waziri huyo ametembelea Kiwanda cha kusarifu Dagaa Kama pamoja na kuangalia majiko ya kushemshia Dagaa Bububu Kijichi.