Habari

ONGEZKO LA MALARIA MJINI SABABU ZATAJWA

    Masheha wa Mkoa wa Mjini Magharib wamesisitizwa kusimamia vyema usafi wa mazingira katika maeneo yao ili kuondokana na mazalia ya mbu wanaosababisha malaria na maradhi mengine.

VIASHIRIA VYA IDADI YA WATU NI MSINGI WA MAENDELEO

    Maafisa mipango wamehimizwa kuangalia viashiria vya idadi ya Watu katika kutoa maamuzi wakati wa utekelezaji wa mipango yao ili Serikali iweze kupanga Bajeti yake kwa usahihi.

TEHAMA KUWATOA VIJANA KATIKA UTEGEMEZI

    Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewataka Viongozi wa Serikali, Sekta Binafsi na Wadau wa maendeleo Nchini kuweka mikakati ya pamoja ya kujenga miundombinu ya Tehama na kuandaa program za kuwawezesha Vijana ili kupunguza utegemezi.

KUWEPO SHERIA YA MAMLAKA SERIKALI MTANDAO KUTAONGEZA UFANISI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria utumishi na utawala bora Mhe Haroun Ali Suleiman amesema lengo la kutungwa Sheria ya Mamlaka ya Serikali Mtandao ni kuweka usimamizi wa masuala ya Teknologia ya Habari na Mawasiliano katika Utumishi wa Umma.

Akiwasilisha mswada wa kufuata Sheria ya Wakala Serikali mtandao No.12 ya Mwaka 2019 na kutunga Sheria ya Mamlaka ya Serikali Mtandao Zanzibar amesema Sheria hiyo itawezesha  kuweka utaratibu mzuri wa uanzishwaji na uwendeshaji wa mifumo ya Kieletronic Nchini.

SERIKALI KUZICHUKULIA HATUA BAA ZINAZOKIUKA SHERIA

Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ imesema itaendelea kuzichukulia hatua za kuzifungia Baa zote ambazo zinakwenda kinyume na utaratibu wa Sheria uliopo.

Akijibu swali la mwakimishi wa jimbo la pandani waziri wa wizara hiyo Mhe. Masoud Ali Mohamed amesema.licha ya uwepo wa Sheria inayotoa muongozo wa kupata Kibali cha kuendesha shughuli. Za. Muziki Sheria hiyo haijaruhusu Baa yoyote kupiga Muziki kwa Sauti. Kubwa na kwa muda zaidi ya Saa Sita Usiku.

WANAFUNZI WA SKULI ZA MSINGI WAMETAKIWA KUWA NA NIDHAMU.

Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Kalli, amewahimiza Wanafunzi wa Skuli za msingi kuwa na Nidhamu wanapokuwa Skuli ili kuwasikiliza Walimu wanapofundisha na kuwa Wanafunzi bora. 

Salum Kalli amesema hayo katika kazi ya kukabidhi Zawadi kwa Wanafunzi wa Shule za msingi Gungu na Kikungu zilizoko Manispaa ya Kigoma Ujiji, ambao wamefanya vizuri katika Masomo yao.

MASHEHA KUSIMAMIA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA MAENEO YAO

Masheha wa Mkoa wa Mjini Magharibi wamesisitizwa kusimamia vyema usafi wa Mazingira katika maeneo yao ili kuondokana na mazalia ya Mbu wanaosababisha Malaria na Maradhi mengine.

SERA MPYA TEHAMA KUIMARISHA MAENDELEO.

Mkurugenzi Idara ya Mawasiliano Dk. Mzee Suleiman Mndewa amesema kufanyiwa marejebisho Sera ya TEHAMA kutasaidia kuimarisha Mipango ya Maendeleo katika Taifa.

Akifungua Kongamano la kujadili Sera mpya ya TEHAMA Mdewa amesema kuwa Sera iliyopo imepitwa na muda hiyo Teknologia inaendelea kukuwa na inahitaji kuwekewa misingi ili iweze  kwenda na wakati wa sasa.

Aneth Kasebele akiwasilisha mada katika Kongamano hilo amesema  Sera inahitaji kuleta tija katika makundi yote katika Jamii .

BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU ZANZIBAR KUFANYA MAGEUZI SHERIA YA MIKOPO

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zaznibar imekusudia kufanya mageuzi wa Sheria ya Mikopo kwa lengo la kutoa fursa kwa Wanafunzi wa Ngazi ya Stashahada kuweza kupata mikopo ya Elimu ya juu na kupata wanufaika wengi zaidi.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa ameyasema hayo huko Chukwani wakati wa Mafunzo ya Mswaada wa Sheria mpya ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.

WATOTO WATAKIWA KUPEWA CHAKULA KULINGANA NA UMRI WAO

     Jamii imetakiwa kuwa na utaratibu  wa kuwapa chakula Watoto kulingana na umri wao ili kuwakinga na maradhi ya utapia mlo.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.