Habari

WAHASIBU NA WAKAGUZI WATAKIWA KUTOA MAFUNZO

   Wahasibu na  Wakaguzi wa Umma  wameshauriwa kutoa Mafunzo katika Taasisi zao ili  kupata Wahasibu wenye uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi pale  wanapohitajika sehemu za Kazi.

   Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wahasibu Wakaguzi na Washauri elekekezi wa kodi Zanzibar ZIAAT CPA Ndg.Ame Burhan Shadhil katika Mkutano wa Wahasibu na Wakaguzi wa Umma amesema ni vyema kwa Wahasibu   waliothibitishwa na wenye CPA kutoa Mafunzo kwa Wahasibu Wadogo ili kuwajengea uwezo wa kufanya kazi sehemu mbali mbali.

WIZARA YA ELIMU YAJIPANGA KUFANYA MAGEUZI

    Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imesema inaendelea kufanya Mageuzi katika Sekta ya Elimu ili kuona Wanafunzi wanapata Elimu iliyo bora.

KAMATI YA USHAURI WA KITAALUMA MJI MKONGWE YAZINDULIWA

    Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga ameitaka Kamati ya Ushauri wa Kitaalamu Scientific Advisory Committee na Cross Cutting Task Team ya Mji Mkongwe kusimamia Sheria na kanuni zilizowekwa ili ziweze kuleta manufaa kwa Jamii na Serikali.

    Akizungumza katika Uzinduzi wa Kamati ya Ushauri wa Kitaaluma Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe .Mudrik Ramadhan Soraga amesema Kamati hizo ni muhimu kushauri miradi ya Mji Mkongwe Jambo ambalo limekuwa likiufanya Mji huo kubaki katika hadhi yake.

RC AYOUB ATOA AGIZO KALI KWA MWEKEZAJI

    Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Ayoub Mohamed Mahamoud, ameuagiza Uongozi wa Kamisheni ya Kazi kuandaa Mikataba ya kazi kwa Wafanyakazi wa Hoteli ya Tsunami Village Limited ya Dongwe ambao hawana Mikataba hiyo.

VIONGOZI WASHIRIKI KUMUAGA LOWASA DAR

   Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Ayoub Mohamed Mahamoud, ameuagiza Uongozi wa Kamisheni ya Kazi kuandaa Mikataba ya kazi kwa Wafanyakazi wa Hoteli ya Tsunami Village Limited ya Dongwe ambao hawana Mikataba hiyo.

DKT. MWINYI ATOA POLE KWA MSIBA WA EDWARD LOWASSA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameungana na Viongozi wa Chama, Serikali na wakaazi wa Jiji la Dar Es Salaam kutoa Mkono wa pole katika Msiba wa aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyai Lowasa.

Akiwa ameambatana na Mkewe Mama Maryam Mwinyi Raisi Mwinyi amemuelezea Hayati Edward Lowasa kuwa ni Kiongozi

SMZ KUSHIRIKIANA NA WADAU WA UTALII KUKUZA SEKTA YA UTALII

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kushirikiana na Wadau wa Utalii ili kukuza Sekta ya Utalii Zanzibar.

Akizungumza katika Kikao cha Wadau wa Utalii Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe Mudrik Ramadhan Soraga amesema hatua hiyo itasaidia kukuza Uchumi wa Nchi na kuleta Maendeleo kupitia Sekta hiyo na kuona Utalii unainufaisha Zanzibar katika Nyanja mbali mbali. 

Waziri Soraga amesema atahakikisha Wanashirikiana na ZRA kuimarisha mifumo ya malipo kwa Kielektroniki yanafanyika ili kuongeza Pato la Serikali.

SHILINGI MILIONI MIA TATU ZIMETOLEWA KWA WAVUVI

Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi imetoa Mgao wa Shilingi Milioni Mia Tatu kati ya Shilingi Bilioni 1 Nukta 3 ya Fedha zinazokusanywa katika hifadhi za Bahari kwa Mwaka 2022/2023.

Akikabidhi Fedha hizo kwa Kamati Nne ikiwemo ya Chabamca ya Malindi, Wilaya ya Mjini, Menai ya Mkoa wa Kusini Unguja, Tumca ya Tumbatu na Mimca ya kaskazini unguja 

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Mhe Shaabani Ali Othman amezitaka kamati hizo kuongeza Wigo na mapato yatokanayo na Hifadhi za Bahari.

JAMII IMESISITIZWA KURIPOTI MATUKIO YA UNANYASAJI WA KIJINSIA.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe Riziki Pembe Juma ameisisitiza Jamii Kuripoti Matukio ya unanyasaji wa Kijinsia kwa Watoto mara wanapoona viashiria vya Unanyasaji.

Amesema wizara hiyo inalaani vitendo vya unyanyasaji wa Kijisia aliofanyiwa Mtoto wa Kike wa Miaka 9 Mkaazi wa Bububu Magengeni aneishi na Mama yake wa Kambo kufatia Taarifa zilizotolewa katika Mitandao ya Kijamii inayonesha kufanyiwa unayanyasaji Mtoto huyo.

Waziri Riziki  amesema endapo Vitendo hivi vikitokezea Sheria itachukua hatua ili haki za Wanawake na Watoto zipatikane. 

HUDUMA YA PATA DAWA NI MUHIMU KWA WATANZANIA

Wizara ya Afya Zanzibar imeitaka Kampuni ya Simu ya Mkononi Tigo Zantel na Laina Finance Limited kuhakikisha wanafuata misingi ya faida inayozingatia Ubinaadamu na sio kukomoa Wananchi katika huduma ya pata dawa.

Naibu Waziri wa Afya Mhe Hassan Khamis Hafidh, ameeleza hayo alipozindua huduma ya PATA DAWA kupitia Simu ya Mkononi Tigo Zantel kwa kushirikiana Laina Finance Limited huko Golden Tulip Uwanja wa Ndege.

Amesema huduma hiyo ni muhimu kwa maisha ya Watanzania kwani Wananchi wengi ni wangonge hivyo ni muhimu kuwasaidia katika mambo mbalimbali.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.