Wahasibu na Wakaguzi wa Umma wameshauriwa kutoa Mafunzo katika Taasisi zao ili kupata Wahasibu wenye uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi pale wanapohitajika sehemu za Kazi.
Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wahasibu Wakaguzi na Washauri elekekezi wa kodi Zanzibar ZIAAT CPA Ndg.Ame Burhan Shadhil katika Mkutano wa Wahasibu na Wakaguzi wa Umma amesema ni vyema kwa Wahasibu waliothibitishwa na wenye CPA kutoa Mafunzo kwa Wahasibu Wadogo ili kuwajengea uwezo wa kufanya kazi sehemu mbali mbali.
Afisa Muandamizi Taasisi ya Wahasibu ,Wakaguzi na Washauri elekekezi Zanzibar ZIAAT Dkt.Khamisi Mbarouk Khamis amesema kupitia Taasisi hiyo itaisaidia Serekali kuwapatia huduma bora Wananchi na kutoa taarifa za hesabu za fedha kwa usahihi kupitia Mafunzo wanayopatiwa Wahasibu na Wakaguzi hao.
CPA Riziki Faki kutoka Shirika la umeme ZECO amesema kupitia Mkutano huo utawajengea uelewa na Uzoefu wa kufanya kazi zao kwa ufanisi.