Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi imetoa Mgao wa Shilingi Milioni Mia Tatu kati ya Shilingi Bilioni 1 Nukta 3 ya Fedha zinazokusanywa katika hifadhi za Bahari kwa Mwaka 2022/2023.
Akikabidhi Fedha hizo kwa Kamati Nne ikiwemo ya Chabamca ya Malindi, Wilaya ya Mjini, Menai ya Mkoa wa Kusini Unguja, Tumca ya Tumbatu na Mimca ya kaskazini unguja
Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Mhe Shaabani Ali Othman amezitaka kamati hizo kuongeza Wigo na mapato yatokanayo na Hifadhi za Bahari.
Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Dk.Aboud Suleiman Jumbe amesema Wizara hiyo itaendelea kutoa ushirikiano na Wadau wa Hifadhi kutimiza malengo ya hifadhi hizo ndani ya Jamii.
Mkurugenzi Idara ya Uhifadhi wa Bahari Dk. Makame Omar Makame amesema Asilimia 30 ya Fedha zinazokusanywa kwenye Hifadhi ndizo zinazogaiwa katika Jamii ili iendelee kuwa na imani na Serikali juu ya umuhimu wa kuhifadhi maeneo ya Bahari.
Wizara ya Uchumi wa Buluu na uvuvi imetoa Mgao wa Fedha hizo kufuatia malalamiko ya Muda Mrefu kwa Wakuu na Wasimamizi wa hifadhi kutopatiwa Mgao kwa muda mrefu.