Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga ameitaka Kamati ya Ushauri wa Kitaalamu Scientific Advisory Committee na Cross Cutting Task Team ya Mji Mkongwe kusimamia Sheria na kanuni zilizowekwa ili ziweze kuleta manufaa kwa Jamii na Serikali.
Akizungumza katika Uzinduzi wa Kamati ya Ushauri wa Kitaaluma Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe .Mudrik Ramadhan Soraga amesema Kamati hizo ni muhimu kushauri miradi ya Mji Mkongwe Jambo ambalo limekuwa likiufanya Mji huo kubaki katika hadhi yake.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mji Mkongwe Ndg.Ali Said Bakari amesema Kamati hiyo inamchanganyiko wa Wataalamu tofauti ambao wataweza kuendelea kuhifadhi na kuendelea haiba ya Mji Mkongwe ambayo ni Urithi wa Taifa .
Mwenyekiti wa Scientific Aadvisory Committee Ndg. Yasser De Costa na Mwenyekiti wa Cross Cutting Task Team Ndg.Mwanaidi Saleh Abdallah wameahidi kushirikiana na Mamlaka ya Mji Mkongwe ili kuendeleza urithi wa Dunia kwa kuhifadhi miundombinu iliyopo .