Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe. Ayoub Mohamed Mahamoud, ameuagiza Uongozi wa Kamisheni ya Kazi kuandaa Mikataba ya kazi kwa Wafanyakazi wa Hoteli ya Tsunami Village Limited ya Dongwe ambao hawana Mikataba hiyo.
Agizo hilo amelitoa kufuatia Mwekezaji wa Hoteli hiyo kushindwa kuwapatia Mikataba Wafanyakazi wake, jambo ambalo ni kinyume na sheria za kazi Mkuu huyo wa Mkoa amesema Serikali haifurahishwi kuona Wawekezaji wanashindwa kufuata sheria za Nchi, hivyo amemtaka Mwekezaji huyo kuhakikisha analipa kodi za Serikali, haki za Wafanyakazi pamoja na Hati ya matumizi ya Ardhi.
Mwekazaji huyo wa Hoteli ya Tsunami Village Limited Bibi Sacha Decina Raia wa Italy, ameahidi kukaa pamoja na Uongozi huo ili kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.
Akizungumza kwa niaba ya Wafanyakazi wenzakeNdg.Jaku Issa amesema wanahangaika sehemu mbali mbali ili kupata haki zao lakini mpaka sasa hawapata mafanikio yoyote kutoka kwa Viongozi wa Hoteli hiyo.
Wakati huo huo Mhe.Ayoub ametembelea maeneo yenye migigoro ya ardhi Paje na Jambiani na kuwataka Wananchi kufuata Sheria za Ardhi.