Habari

WAFANYAKAZI ZRA WAPEWA MAFUNZO

    Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar kwa Pemba wametakiwa kufuata kanuni za Utumishi wa Umma pamoja na maadili ya kazi zao ili kuweza kutoa huduma kwa ufanisi.  

   Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na utawala ZRA Ndg.Seif  Suleiman Ali katika Mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi wa ZRA Pemba huko Ofisini kwao Gombani Chake Chake.

    Amesema Mafunzo hayo yamelenga kuongeza ufanisi kwa Watendaji hao na kuweza kuwahudumia walipa kodi kwa ufanisi.

MAJALIWA ATOA RATIBA MAZISHI YA LOWASA

    Mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Edward Lowasa unatarajiwa kuzikwa Tarehe 17/2/2024 Kijini kwao Wilayani Monduli Mkoani Arusha. 

   Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu Kassim Majaaliwa wakati akitoa ratiba ya Mazishi ya  aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward  Lowasa  Nyumbani kwake Jijini Dar es salaam amesema Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza Mazishi hayo.

BOTI ZA KISASA ZAWAFIKIA WAKULIMA WA MWANI PEMBA

    Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe.Shaaban Ali Othman amekabidhi Boti  140 kwa Wakulima wa Mwani na Wajasiriamali Kisiwani Pemba, kupitia Mkopo wa mfuko wa Ahuweni 19,  ili ziweze kusaidia katika harakati zao za Baharini.

   Akikabidhi Boti hizo huko katika Afisi za Wizara ya Uchumi wa Buluu Wete, Mhe.Shaaban amesema Boti hizo zimegharimu kiasi kikubwa cha fedha , huku Serikali ikiamini kuwasaidia Wananchi wake kujikwamua  kupitia Boti hizo .

ZBC YATILIANA SAINI NA POSTA

    Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC limetiliana Saini na Shirika la Posta Tanzania ili kushirikiana katika kutowa  huduma kwa Jamii.

Utiaji Saini huo uliofanyika katika Ukumbi wa  Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC, uliowashirikisha Watendaji na Viongozi wa Shirika la ZBC  na  Shirika la Posta.

MKUTANO WA MADAKTARI BINGWA KUFUNGULIWA

    Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk.Philip Isdor Mpango amesema ili kuhakikisha Tanzania inaendana  na mabadiliko ya huduma za Afya imejipanga kuwekeza kupitia Hospitali zake.

    Akifungua Mkutano wa Madaktari Bingwa wa moyo Afrika amesema mpango huo umezingatia zaidi kuwa na vifaa vya kisasa na kusomesha Madaktari wake kwa idadi kubwa ili kutosheleza katika kuwafikia Wananchi.

NEEMA TUPU ZIARA YA RAIS WA POLAND NCHINI TANZANIA

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan. Amesema Tanzania itaendeleza ushirikiano na Taifa la Poland katika mipango ya maendeleo kupitia Sekta za kimkakati zikiwemo Biashara na uwekezaji.

    Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mapokezi rasmi na kuwa na mazungumzo ya faragha na Rais wa Poland Andrezej Duda aliewasili Nchini jana Raisi Samia amesema Ziara ya Rais duda ni kielelzo cha kuimarisha fursa za uwekezaji katika Sekta za Tehama, Kilimo, Utalii, Usimamizi wa Taka Uchumi wa Kidigitali na Uchumi wa Buluu.

ZRA KUWATAKA MAWAKALA KUSIMAMIA ULIPAJI WA KODI

     Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ZRA Ndg. Yussuf Juma Mwenda amewataka Mawakala walioruhusiwa kuingiza vileo Zanzibar kuhakikisha wanasimamia ulipaji wa kodi kikamilifu.

    Akizungumza na Mawalaka hao Kamishna Mwenda amesema kuwa wanawajibu wa kuhakikisha Mapato ya Serikali yanapatikana na kuongezeka.

    Amewahakikishia kuwa Mamlaka ya Mapato itafanya kila juhudi kuona kuwa Mawakala hao wanatekeleza vyema majukumu yao ili Serikali iendelee kupata Mapato.

UTUNZAJI WA MAZINGIRA WATAKIWA KUZINGATIWA KWA WAMILIKI WA VIWANDA

   Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Ndg.Ahmed Abuubakar Mohammed, amewataka Wamiliki wa  Viwanda kuzingatia utunzaji wa mazingira na afya za Wafanyakazi ili kuepukana na athari zinazoweza kujitokeza.

   Ametoa kauli hiyo huko Vitongoji Kisiwani Pemba katika Ziara ya kukagua Kiwanda cha Kokoto na Kiwanda cha kuhifadhi na kuchoma taka za Hospitali,  Amesema Serikali kupitia Mamlaka ya usimamizi wa mazingira imeandaa

MEGAWATI 49.5 ZA UMEME KWA NGUVU YA MAJI KUONDOA TATIZO LA UMEME

    Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imesaini Makubaliano ya Mkataba na Kampuni ya Dongfang Electric International Corporation ya Nchini China Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Kituo cha  uzalishaji Umeme kwa nguvu ya Maji katika Mto Malagarasi Mkoani Kigoma huku  ikiahidi kumaliza  tatizo la kukosekana kwa  Umeme Nchini.

   Akizungumza mara baada ya kushuhudia kusainiwa kwa Mkataba huo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe.Doto Biteko amesisitizia usimamizi wa Mradi huo.

KITUO CHA KULELEA WATOTO YATIMA CHAFUNGULIWA

    Ushirikiano wa Serikali na Taasisi Binafsi wa kuwaenzi Watoto Yatima utasaidia kuwawezesha Watoto hao kuwa katika misingi imara.

    Akizungumza katika Ufunguzi wa Kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Rahma al Khair Education Compelex Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Riziki Pembe Juma amesema Taasisi Binafsi zimekuwa na mchango katika kujenga Vituo vya kulelea Watoto Yatima ambapo huisaidia Serikali na Jamii kupunguza Watoto wenye mazingira magumu.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.