Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar kwa Pemba wametakiwa kufuata kanuni za Utumishi wa Umma pamoja na maadili ya kazi zao ili kuweza kutoa huduma kwa ufanisi.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na utawala ZRA Ndg.Seif Suleiman Ali katika Mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kiutendaji Watumishi wa ZRA Pemba huko Ofisini kwao Gombani Chake Chake.
Amesema Mafunzo hayo yamelenga kuongeza ufanisi kwa Watendaji hao na kuweza kuwahudumia walipa kodi kwa ufanisi.
Mkurugenzi huyo wa Utawala wa ZRA ametoa wito kwa Watumishi hai kuyatumia Mafunzo katika kazi zao.
Naye kwa upande wake Meneja utawala wa ZRA Pemba Ndg.Abeid Omar Salum amesema Mafunzo hayo yatawawezesha Wafanyakazi hao kujua haki na wajibu wao.
Wakizungumzia Mafunzo hayo baadhi ya Wafanyakazi wa ZRA Pemba wameshukuru kwa Ofisi yao kuwapatia Mafunzo hayo kwani ni muhimu.