ZRA KUWATAKA MAWAKALA KUSIMAMIA ULIPAJI WA KODI

ZRA

     Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ZRA Ndg. Yussuf Juma Mwenda amewataka Mawakala walioruhusiwa kuingiza vileo Zanzibar kuhakikisha wanasimamia ulipaji wa kodi kikamilifu.

    Akizungumza na Mawalaka hao Kamishna Mwenda amesema kuwa wanawajibu wa kuhakikisha Mapato ya Serikali yanapatikana na kuongezeka.

    Amewahakikishia kuwa Mamlaka ya Mapato itafanya kila juhudi kuona kuwa Mawakala hao wanatekeleza vyema majukumu yao ili Serikali iendelee kupata Mapato.

    Aidha Kamishna Mwenda amekemea vitendo vya kuingiza bidhaa hiyo kwa njia ya Magendo.

   Nao Mawakala  wamemthibitishia kuwa watajitahidi kutekeleza wajibu wao na kulipa kodi kwa lengo la kuleta maendeleo ya Nchi.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.