Habari

ZURA YATAJA SABABU YA ONGEZEKO LA BEI YA MAFUTA

   Mamlaka ya udhibiti huduma za Maji na Nishati Zanzibar ZURA imetangaza kuongezeka kwa Bei za Mafuta kwa Mwezi wa February 2024 zitakazoanza kutumia Ijumaa ya Wiki hii.

    Akitangaza Bei hizo kwa Waandishi wa Habari Meneja Kitengo cha Uhusiano ZURA Ndg.Mbarak Hassan Haji amesema kupanda kwa bei hiyo kunatokana na kuongezeka kwa gharama ya uingizaji Mafuta katika Bandari ya Dar es salama na Tanga

BILLIONI 60 ZATUMIKA UNUNUZI WA VIFAA TAASISI YA MOYO

   Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete imeandaa Mkutano wa Kimataifa utakaoambatana na Mafunzo Maalum ya Matibabu ya Moyo ili kuongeza Utaalamu utakaoimarisha zaidi huduma za matibabu

   Akitoa taarifa Mkurugenzi Mtendaji Taasisi hiyo Dkt Peter Kisenge Amesema Mkutano huo utashirikisha Wataalamu wa Mataifa 40 wakiwemo Madaktari Bingwa una lengo la kuitangazaTanzania kuwa kimbilio la Matibabu ya Moyo 

WAZIRI WA UCHUMI WA BULUU NA UVUVI AAPISHWA

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemuapisha Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar Mhe. Shaaban Ali Othman kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango Zanzibar, hafla iliyofanyika Ikulu Zanzibar.

    Mhe. Shaaban Ameapishwa kwa mujibu wa Sheria ya Tume ya Mipango nambari 3 ya Mwaka 2012, Ambapo inamtaka Mjumbe wa Tume ya Mipango Kuapa Kiapo cha Uaminifu katika kutekeleza Kazi za Mjumbe wa Mipango Zanzibar. 

 

UWEKEZAJI UNAHITAJI KUWEPO KWA MIFUMO IMARA YA UTOAJI HAKI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema uwekezaji wa Miradi ya Kiuchumi unahitaji uwepo Mifumo imara wa utoaji haki.

SERIKALI ZOTE MBILI ZINAUNGA MKONO JUHUDI ZA SEKTA BINAFSI.

Waziri wa Ujenzi  Mawasiliano na Uchukuzi Dr Khalid Salum Mohammed  amesema Serikali zote mbili zinaunga Mkono juhudi za Sekta Binabsi kwa kuendana na Sera za Serikali katika kufikia mabadiliko ya Kidigitali.

WAFANYAKAZI KUZINGATIA SHERIA ZA KAZI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar, Mhe Ali Suleiman Ameir amewataka Watendaji wa Ofisi hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ili kufikia malengo na matarajio ya Serikali.

Akizungumza na Wakuu wa vitengo wa Ofisi ya Rais Ikulu wakati wa kujitambulisha mara baada ya kuteuliwa hivi karibuni amesema ni vyema kwa Watendaji kutekeleza Majukumu yao ya Msingi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ili kufikia maendeleo endelevu.

WAZIRI SORAGA AKABIDHIWA WIZARA

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Mudriq Ramadhan Soraga amesema ataweka Mkazo katika maeneo muhimu ya Utalii ikiwemo Uwanja wa Ndege na uwekezaji ili kuongeza Mapato ya Nchi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Wizara hiyo hapo Kikwajuni ahidi kuendeza ufanisi zaidi.

Akikabidhi kwa Waziri Soraga, Mh Simai Mohamed Said amewaomba Watendaji wa Wizara hiyo kumpa ushirikiano Waziri ili kuendeleza majukumu yao. 

JAMII IMEHIMIZWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA SEKTA YA AFYA

Jamii imehimizwa kuunga Mkono juhudi za Serikali za kuimarisha Sekta ya Afya kwa kujitokeza kuchangia Damu salama ili kupunguza idadi ya Vifo vya Mama na Mtoto wakati wa kujifungua.

Akifungua Kampeni ya kuchangia Damu salama Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la utangazaji Zanzibar ZBC Ramadhan Bukini amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza idadi kubwa ya vifo vya Wakinamama hao ambao wamekuwa wakipungukiwa na Damu wakati wa kujifungua na kusababisha kupoteza Maisha yao.

MAWAKILI WAPYA ZANZIBAR WAPEWA NASAHA

    Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Khamis Ramadhan Abdallah amewataka Mawakili wapya kutekeleza kazi zao kwa kufuata sheria na taaluma.

     Akizungumza katika Ukumbi wa Mahakama Kuu Tunguu wakati wa kuwaapisha Mawakili Wapya kumi na sita ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya Wiki ya Sheria Zanzibar. Amesema maadili ya kazi zao ni kusimamia haki na wajibu ili kutetea haki za Wananchi na kuisaidia Mahakama kutenda haki kwa Wananchi.

TAKUKURU YABAINI KASORO MIRADI KINONDONI

    Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni imebaini kasoro katika Miradi minne yenye thamani ya Shilingi Bilioni 7 nukta 2 katika Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar- es-salaam.

   Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni Ndg.Ismail Suleiman wakati akitoa Taarifa ya Utendaji wa Taasisi hiyo katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2023.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.