ONGEZKO LA MALARIA MJINI SABABU ZATAJWA

WIZARA YA AFYA NA MASHEHA MJINI

    Masheha wa Mkoa wa Mjini Magharib wamesisitizwa kusimamia vyema usafi wa mazingira katika maeneo yao ili kuondokana na mazalia ya mbu wanaosababisha malaria na maradhi mengine.

    Akifungua Mkutano kwa Masheha wa Mkoa wa Mjini Magharibi unaohusiana na hali ya Malaria Nchini Mkuu wa Kitengo cha Elimu ya Afya kutoka Wizara ya Afya Ndg.Bakari Magarawa amesema kwa sasa Wilaya ya Mjini inaongoza kwa Malaria kutokana na kuwepo kwa sababu mbali mbali zikiwemo mabadiliko ya Tabianchi pamoja na hali ya Mazingiza, hivyo amewataka Viongozi hao wa Shehia kusimamia usafi ili kuondokana na Maradhi hayo

    Akizungumzia suala la Macho mekundu Ndg.Magarawa amewataka Masheha hao kuwaelimisha Wananchi kutotumia Dawa zisizo rasmi kutibu Macho na badala yake kufika katika vituo vya Afya kupata matibabu ya Maradhi hayo

    Afisa Afya ya Jamii kutoka Wizara ya Afya Programu ya kumaliza Malaria Zanzibar Ndg.Mwinyi Khamis amesema imeripotiwa kuwa zaidi ya Wagonjwa elfu tano wa Malaria mwaka huu

    Sheha wa Shehia ya Malindi Ndg.Hassan Masoud Ali na Sheha wa Shehia ya Sebleni Mohamed Mussa wamesema watahakikisha wanasimamia vyema suala la usafi wa mazingira katika Shehia zao ili kuondokana na mazalio ya Mbu.

 

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.