Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara maalum za SMZ imesema itaendelea kuzichukulia hatua za kuzifungia Baa zote ambazo zinakwenda kinyume na utaratibu wa Sheria uliopo.
Akijibu swali la mwakimishi wa jimbo la pandani waziri wa wizara hiyo Mhe. Masoud Ali Mohamed amesema.licha ya uwepo wa Sheria inayotoa muongozo wa kupata Kibali cha kuendesha shughuli. Za. Muziki Sheria hiyo haijaruhusu Baa yoyote kupiga Muziki kwa Sauti. Kubwa na kwa muda zaidi ya Saa Sita Usiku.
Mapema Spika wa Baraza la Wawakilishi Mh. Zubeir Ali Maulid amemuapisha Mhe Sharif Ali Sharif kuwa Mjumbe wa baraza hilo kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi hivi Karibuni.
Katika hatua nyengine Mhe. Zubeir amelitaarifu Baraza kuwa miswaada 6 ya Sheria iliopitishwa katika mkutano wa 13 sasa imekuwa Sheria kamili baada ya kusainiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.