Akimwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Katika maadhimisho ya Miaka 100 ya kuazishwa kwa Skuli ya Benbella, huko Uwanja wa Mnazi Mmoja, Waziri wa Maendeleo ya Jamaii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe.Riziki Pembe Juma, Amesema Sekta ya Elimu inamchango mkubwa wa kuleta mageuzi Nchini.
Amesema hatua ya Wizara ya Elimu kuifanya Skuli ya Benbella kuwa maalum kwa ajili ya Wanawake, ilikuwa na lengo la kutoa fursa kwa Watoto wa Kike wasiendele kubaki nyuma katika suala la kujitafutia Elimu.
Aidha akizungumza suala la udhalilishai Mhe.Riziki amewataka Walimu kuwasimamia Wanafunzi ili kukabiliana na vitendo hivyo huku akiwasisitiza Wanafunzi hao kuwa waangalifu kutokana na vishawishi vilivyoenea katika Jamii.
Wanafunzi waliosoma Skuli hiyo, wameahidi kusaidia Skuli hiyo ili kuendelea kutoa Wasomi wazuri na wenye fani mbali mbali kwa maendeleo ya Taifa.
Nao Wanafunzi walisoma katika Skuli hiyo, wamesema wataendelea kuisaidia ili iendelee kutoa Wataalamu wa fani mbali mbali.
Mwenyekiti wa Kamati ya maadhimisho hayo, Ndg.Ramla Mohamed Ramadhan, akitoa historia ya Skuli ya Ben bella, amesema Skuli hiyo ilianzishwa Mwaka 1924 ambayo wakati huo ikijulikana kama Commercial na baadae kubadilishwa Jina na kuitwa Ben-Bella kwa kumuenzi muasisi wa Taifa la Algeria, Marehemu Ahemd Benbella.