KAMATI BLW HAIRIDHISHWI NA JENGO LA BARAZA LA MITIHANI.

BARAZA LA WAWAKILISHI

Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wakilishi imesema hairidhishwi na Mazingira ya Jengo la Ofisi za Baraza la Mitihani

Kutokana na umuhimu wake na hali iliokuwa nayo.

Akiwasilisha  Ripoti ya Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wakilishi  kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Mwenyekiti, wa Kamati hiyo Mhe Sabiha Filfil Thani amesema hali ya Jengo kwa sasa  ni chakavu na haliko katika Mazingira rafiki hivyo ni vyema kufanyiwa matengenezo ili liendane na Ofisi za kisasa na lenye kuridhisha.Hata hivyo Kamati imeipongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali  na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume KIST kwa kuweka utaratibu maalum wa Wanafunzi wanaotoka Skuli hizo  kuendelea na masomo yao katika Taasisi hiyo kwa kuwapunguzia gharama za malipo ya  Masomo wakati wanapo soma Chuoni hapo.

Wakitoa maoni  ya Ripoti ya Kamati ya Ustawi wa Jamii Wajumbe hao wameishauri Serikali kulifanyia haraka suala la uhaba wa Madaktari hasa katika Hospital mpya za Wilaya zilizo funguliwa hivi karibuni.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.