Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wakilishi imesema hairidhishwi na Mazingira ya Jengo la Ofisi za Baraza la Mitihani
Kutokana na umuhimu wake na hali iliokuwa nayo.
Akiwasilisha Ripoti ya Kamati ya Ustawi wa Jamii ya Baraza la Wakilishi kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 Mwenyekiti, wa Kamati hiyo Mhe Sabiha Filfil Thani amesema hali ya Jengo kwa sasa ni chakavu na haliko katika Mazingira rafiki hivyo ni vyema kufanyiwa matengenezo ili liendane na Ofisi za kisasa na lenye kuridhisha.Hata hivyo Kamati imeipongeza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume KIST kwa kuweka utaratibu maalum wa Wanafunzi wanaotoka Skuli hizo kuendelea na masomo yao katika Taasisi hiyo kwa kuwapunguzia gharama za malipo ya Masomo wakati wanapo soma Chuoni hapo.
Wakitoa maoni ya Ripoti ya Kamati ya Ustawi wa Jamii Wajumbe hao wameishauri Serikali kulifanyia haraka suala la uhaba wa Madaktari hasa katika Hospital mpya za Wilaya zilizo funguliwa hivi karibuni.