SERIKALI KUENDELEA KUJENGA MIUNDOMBINU KATIKA MAENEO YA UTALII

RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Hussein Ali Mwinyi  amesema Serikali itaendela kujenga Miundombinu  katika maeneo ya Utalii  ili Wananchi waweze  kufanya shughuli zao kwa  uhakika.

Akifungua Mkutano wa pili wa Wadau wanaouza Bidhaa za Utalii kutoka Nchi mbali mbali Duniani, huko Golden Tulip Uwanja wa Ndege,amesema Miundo Mbinu hiyo itaongeza ukuaji wa Uchumi na pato la Taifa.

Aidha Dk.Mwinyi, amesema Sekta ya Utalii inaongoza  katika kukuza pato la Taifa,hivyo Serikali itaendelea kushirikiana na Sekta Binafsi ili kufanikisha maendeleo ya Kiuchumi yanazidi kuimarika.

Amesema sekta ya Utalii itaongeza Biashara na kuinua kipato cha Mwananchi kupitia Sekta ya Anga, pamoja na kumnufaisha Mwananchi mmoja mmoja kwa  kuuza  Bidhaa zao.

Pia amewataka Wananchi wachangamkie fura mbali mbali zikiwemo za kusafirisha Watalii.

Nae Waziri wa Utalii na mambo ya kale Mh Mudriq Ramadhan Souraga, amesema  sekta ya Utalii kwa sasa ipo vizuri na ameahidi kuimarisha baadhi ya mambo ya utalii.

Mwenyekiti wa Mkutan huo Rahim Bhaloo na Ofisa Mtendaji Mkuu Benki ya Exim Bwana Jafar Mtundu na muandaaji Mkuu wa Mkutano huo  bwana Dominot shoo kwa pamoja wamesema   lengo kuu ni kuwaleta Wadau wanaotaka huduma na watoa huduma ili kuongeza wigo  na kuzidi kuimarika.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.