Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendela kujenga Miundombinu katika maeneo ya Utalii ili Wananchi waweze kufanya shughuli zao kwa uhakika.
Akifungua Mkutano wa pili wa Wadau wanaouza Bidhaa za Utalii kutoka Nchi mbali mbali Duniani, huko Golden Tulip Uwanja wa Ndege,amesema Miundo Mbinu hiyo itaongeza ukuaji wa Uchumi na pato la Taifa.
Aidha Dk.Mwinyi, amesema Sekta ya Utalii inaongoza katika kukuza pato la Taifa,hivyo Serikali itaendelea kushirikiana na Sekta Binafsi ili kufanikisha maendeleo ya Kiuchumi yanazidi kuimarika.
Amesema sekta ya Utalii itaongeza Biashara na kuinua kipato cha Mwananchi kupitia Sekta ya Anga, pamoja na kumnufaisha Mwananchi mmoja mmoja kwa kuuza Bidhaa zao.
Pia amewataka Wananchi wachangamkie fura mbali mbali zikiwemo za kusafirisha Watalii.
Nae Waziri wa Utalii na mambo ya kale Mh Mudriq Ramadhan Souraga, amesema sekta ya Utalii kwa sasa ipo vizuri na ameahidi kuimarisha baadhi ya mambo ya utalii.
Mwenyekiti wa Mkutan huo Rahim Bhaloo na Ofisa Mtendaji Mkuu Benki ya Exim Bwana Jafar Mtundu na muandaaji Mkuu wa Mkutano huo bwana Dominot shoo kwa pamoja wamesema lengo kuu ni kuwaleta Wadau wanaotaka huduma na watoa huduma ili kuongeza wigo na kuzidi kuimarika.