Jumla ya Ddola Laki Mmoja na Ishirini zimetumika kununulia vifaa vya Mmatibabu vitakavyotumika katika Hospitali Kkumi na Moja katika Jimbo la Uzini.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa Viongozi wa Jimbo la Uzini, Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Muzdalifa Ndg.Farouk Hamad ameiomba Serikali kuendelea kuisaidia Jumuiya hiyo na kushirikiana nao, ili waweze kuleta misaada zaidi.
Ndg.Farouk amesema Vifaa hivyo vitasaidia kupunguza shida ya upatikanaji wa vifaa tiba na kuwafanya watendaji wa Sekta ya Afya kufanyakazi vyema.
Akipokea msaada wa vifaa hivyo, huko Kituo cha Afya Bambi, Mbunge wa Jimbo la Uzini Mhe.Khamis Hamza Chilo, amewataka Madaktari na Wasimamizi wa Vituo vya Afya kuvitumia vizuri ili lengo liweze kufikiwa.
Amesema vifaa vya Matibabu vilivyotolewa na Jumuiya ya Muzdalifa Charitable ni msaada wenye gharama kubwa hivyo ni vyema vikatumiwa kwa walengwa kama ilivyokusudiwa.
Nao Wananchi wa Kijiji cha Bambi wamewashukuru kwa kuwapatia vifaa hivyo ambavyo wanaimani vitasaidia kwa kiasi kikubwa Wananchi wa Kijiji hicho.
.