TANZANIA KUANDIKA HISTORIA MATUMIZI YA TRENI YA UMEME

MKURUGENZI WA SHIRIKA LA RELI TANZANIA

Kwa mara ya kwanza Tanzania imeandika Historia kupitia Shirika la Reli la Tanzania kwa kufanya majaribio ya kwanza ya kawaida ya Treni yake ya kisasa ya SGR inayotumia Umeme kutoka Dar Es Salaam hadi Mkoani Morogoro.

Treni hiyo ambayo ni ya kwanza kwa Afrika Mashariki inayotumia Umeme ambapo huduma Rasmi ya Safari zake zinatarajiwa kuanza Mwishoni mwa Mwezi wa Julai 2024.

Akizungumza na Wandishi wa Habari Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania Masanja Kadogosa amesema hatua hii ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia ambae aliagiza hadi ifikapo Mwisho wa Mwezi wa Saba 2024 Treni hiyo iwe imeanza kufanya Kazi.

Aidha Mkurugenzi huyo amewatoa hofu Wananchi juu ya changamoto ya   kukatika kwa Umeme na kusema kuwa uendeshaji wa Treni hiyo hakutaathiriwa na kukatika kwa umeme.

Nae Mkurugenzi wa Idara Habari maelezo ambae pia ni Msemaji wa Serikali amesema hatua hiyo ni uthibitisho kwamba kile kilichoahidiwa na Mh Rais kinaenda kutokea na kusema kuna kila sababu ya kujivunia mafanikio yaliyopatikana katika Miradi mikubwa ya kimkakati wakishuhudia uzinduzi wa majaribio hayo wahariri wa Habari na Watendaji wa shirika hilo wakionyesha furaha zao na hapa wanaeleza 

Ujenzi wa reli ya kisasa ya awamu ya kwanza kati ya Dar Es Salaam hadi morogoro ni (km 300) ulizinduliwa  Rasmi  na  Rais  wa awamu ya tano hayati John Pombe Magufuli mwaka 2017 na kimegharimu zaidi ya Shilingi 2.7 Trilioni.   

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.