Waziri Mkuu wa Tanzania amewagiza Watendaji wa Wizara ya Madini kufika Wilaya ya Tarime Vijijini kuzungumza na Wananchi ili kutatua tatizo la fidia ambalo linawasumbua kwa muda mrefu na kuonekana wao Wakimbizi katika ardhi yao.
Akizungumuza na Wananchi katika eneo la Nyamwaga baada ya kusikiliza Kero hizo kutoka kwa Wananchi waliokuwa wakizungumzia suala la fidia zinatolewa na Mgodi wa Barick North Mara.
Awali akizungumza katika Mkutano huo Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mhe Mwita Waitara amesema Wananchi wa Vijiji vinayozunguka Mgodi huo wakipata matatizo ya kutokulipwa fidia za maeneo yao ambayo yamechukuliwa na Wananchi hao kushindwa kulipwa fidia stahiki huku Mbunge wa Viti maalumu Chadema Esther Matiko akisisistiza juu ya malipo hayo kwa Wananchi wa eneo hilo.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema Serikali imeunda Tume ya Kimkakati ya Mawaziri Nane wanao tatua Matatizo ya Wananchi wanaoishi Pembezoni mwa hifadhi na kuahidi Timu hiyo itafika katika vijiji vinavyo zunguka hifadhi ya Taifa ya Serengeti ili kutatua matatizo ya Wananchi hao.