WAANDISHI WA HABARI KUTUMIA KALAMU ZAO KULETA MABADILIKO

BODI YA WAKURUGENZI LATRA

Waandishi wa Habari Nchini wameshauriwa kutumia Kalamu zao kuleta mabadiliko kwani Jamii inaamini kuwa Nguvu ya Kalamu zao inaweza kusaidia kujenga Taifa lenye kuzingatia Utu, Uadilifu, Amani na Utulivu.    

Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Latra Wakili Tumaini Silaa katika Semina ya kuwajengea uwezo Wanahabari Mabalozi iliyofanyika Kibaha Mkoani Pwani na kuongeza kuwa Mamlaka hiyo, imejipambanua kuheshimu na kutoa ushirikiano kwa Wanahabari Nchini.

Akifafanua kuhusu malalamiko ya wananchi juu ya upandaji na ushukaji wa Nauli Kaimu Mkurugenzi udhibiti Uchumi Mamlaka ya udhibiti usafiri wa Ardhini Fahamueli Mkeni ameeleza kuwa kuna gharama mbalimbali za uzalishaji ambazo zinaangaliwa kwa mujibu wa Sheria za Latra. 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.