Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa ametoa Wiki moja kwa Taasisi ya Takukuru na Mkurungrzi wa Halmashauri ya Rorya kuhakikisha wanakamilisha uchunguzi wa wizi wa vifaa vya Skuli uliofanywa na Mwalimu wa Skuli ya Msingi Kinesi 'b' Wilayani Rorya.
Kauli hiyo ameitoa katika mwendelezo wa Ziara yake Mkoa wa Mara Waziri Majaaliwa ameagiza kukamika kwa uchunguzi huo ili kubaini ubadhilifu uliojitokeza katika Ujenzi wa Skuli hiyo ya Msingi Kinesi 'b'.
Mbunge wa Jimbo la Rorya amesema wanakabiliwa na tatizo la Maji katika Halmashauri hiyo licha ya kuwa na Ziwa Victoria kuwa ndani ya Halmashauri hiyo .
Akitoa ufumbuzi wa tatizo hilo la maji katika Wilaya hiyo Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amesema Wizara inatoa fedha kiasi cha Shilingi Milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa chujio la maji ili kupatikana kwa maji safi na salama kwa Wakaazi hao huku Waziri Mkuu akisisitiza kuhusu upatikanaji wa maji safi na salama.