MWAMBA WA MAGEUZI WANANCHI WAMLILIA

 Wananchi Mangapwani

    Wananchi wamesema  Tanzania imepoteza  Kiongozi  muhimu  katika Taifa Marehemu Ali Hassan Mwinyi ambae amejitoa  kuipigania Nchi ili kukuwa  na kusababisha kufunguka kiuchumi kupitia sera ya uwekezaji na kupiga hatua za maendeleo.

    Wakizungumza kwa masikitiko na huzuni kubwa kwa kuondokewa na Kiongozi huyo Wananchi hao wamesema Marehemu Ali Hassan Mwinyi katika uhai wake alikuwa Mtu mwenye kupenda Watu ,kuunganisha Watu  pia  alikuwa ni Mtu  asiyependa kujikweza jambo lililowapa nafasi hata Watu  wa chini kuwa karibu na Kiongozi huyo.

    Aidha wamesema  ni vyema kuyaendeleza  maono ya Mzee huyo ili Taifa lizidi kupiga  hatua za kimaendeleo Nchini. 

    Alhaji  Ali Hhasani Mwinyi amefariki  Siku ya Ijumaa Febuar 29 katika Hospitali ya  Mzena Jijini Dar es salaam na Maiti hiyo kusafirishwa hadi  Visiwani Zanzbar  ambapo Majira ya Saa  Kumi na Mbili Jioni  Maiti hiyo amewasili na kufikishwa katika Kijiji cha  Bweleo  na kuagwa kiheshima na Viongozi mbalimbali  katika Uwanja wa Amani  na kusaliwa  masjid Jamii Zinjibar na hatimae kupelekea katika  makaazi yake ya milele  katika Kijiji cha Manga Pwani.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.