Wananchi wamesema Tanzania imepoteza Kiongozi muhimu katika Taifa Marehemu Ali Hassan Mwinyi ambae amejitoa kuipigania Nchi ili kukuwa na kusababisha kufunguka kiuchumi kupitia sera ya uwekezaji na kupiga hatua za maendeleo.
Wakizungumza kwa masikitiko na huzuni kubwa kwa kuondokewa na Kiongozi huyo Wananchi hao wamesema Marehemu Ali Hassan Mwinyi katika uhai wake alikuwa Mtu mwenye kupenda Watu ,kuunganisha Watu pia alikuwa ni Mtu asiyependa kujikweza jambo lililowapa nafasi hata Watu wa chini kuwa karibu na Kiongozi huyo.
Aidha wamesema ni vyema kuyaendeleza maono ya Mzee huyo ili Taifa lizidi kupiga hatua za kimaendeleo Nchini.
Alhaji Ali Hhasani Mwinyi amefariki Siku ya Ijumaa Febuar 29 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam na Maiti hiyo kusafirishwa hadi Visiwani Zanzbar ambapo Majira ya Saa Kumi na Mbili Jioni Maiti hiyo amewasili na kufikishwa katika Kijiji cha Bweleo na kuagwa kiheshima na Viongozi mbalimbali katika Uwanja wa Amani na kusaliwa masjid Jamii Zinjibar na hatimae kupelekea katika makaazi yake ya milele katika Kijiji cha Manga Pwani.