UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAAZI FUMBA KUANZA KARIBUNI

 Ujenzi Nyumba

     Kampuni  ya Ishirini na Nne Kumi Clobal (2410) kutoka Uturuki inatarajia kuanzisha mradi wa ujenzi wa nyumba za maakazi ili jamii iweze kuishi  katika mazingira bora.

    Akizungumza na Waandishi wa Habari Mwenyekiti  wa mradi huo Tolga Tugtekin amesema  Nyumba hizo za kisasa zitakuwa katika maeneo ya Fumba ambapo Kampuni hiyo inafungua milango kwa Wananchi  kuweza kununua Nyumba hizo mradi utakapokamilika. 

    Amesema kutokana na maono ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Hussein Ali Mwinyi ya kuwaletea maendeleo Wananchi wake  ikiwa ni pamoja na makaazi bora ambapo Kampuni hiyo imehamasika na kuleta uwekezaji wa aina hiyo.

    Waziri wa Biashara na maendeleo ya Viwanda Mh.Omar Said Shaaban amesema Serikali baada ya kusaini sheria mpya ya uwekezaji  imezidi kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza katika miradi mbali mbali ya maendeleo.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.